Serikali yajipanga kutoa pesheni kwa wazee Tanzania

Na Catherine Sungura, MOHSW, Lindi SERIKALI imesema inaendelea kukamilisha taratibu zitakaowezesha utekelezaji wa suala la kutoa pensheni jamii kwa wazee ili liwe endelevu kulingana na mustakabali wa maisha ya wazee wa Tanzania. Kauli hiyo imetolewa leo mjini hapa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Lucy Nkya kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wazee duniani yaliyofanyika …

CCM yafunga kampeni za uchaguzi Igunga

Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa leo alifika mjini Igunga kwa ajili ya kufunga kampeni za CCM kesho kwenye Viwanja vya Sokoni, Kata ya Nkinga. Pichani, Mkapa akiwasili kwenye Hotel ya Peak mjini Igunga jana jioni. (Picha na Bashir Nkoromo)

Mtalii mwingine atekwa Kenya

MTALII mmoja mwanamke wa nchini Ufaransa ametekwa na kundi la watu waliokuwa na silaha karibu na mji wa Lamu, nchini Kenya. Tukio hilo limetokea majuma matatu tu baada ya watalii wawili kutoka Uingereza kushambuliwa piya huko Kiwayu, kaskazini zaidi ya mwambao wa Kenya. Wanaume waliokuwa na silaha walimpiga risasi mwanamume wa Kingereza na kumteka nyara mkewe, ambaye anafikiriwa anazuwiliwa nchini …

Bomoa bomoa ya Dk. Magufuli balaa!

Na Mwandishi Wetu ALAMA za bomoa bomoa (X) zinazowekwa kwa baadhi ya nyumba zilizojengwa kwenye eneo la hifadhi ya barabara limesambaa eneo kubwa nchini, yakiwemo maeneo ya miji midogo-zoezi ambalo endapo litatekelezwa huenda likawaumiza Watanzania wengi maeneo anuai. Kwa mujibu wa uchunguzi ambao mtandao huu umeufanya hadi sasa katika mikoa ya Mara, Morogoro, Iringa, Mbeya, Kagera, Kilimanjaro, Arusha, Rukwa, Mwanza …