Mnyika azindua Tawi la Chadema Sinza ‘C’

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amezindua Tawi Jipya la Chama hicho lililopo eneo la Sinza ‘C’. Tawi hilo lililopewa jina la Msingi wa Ukombozi No 1 lilifunguliwa juzi na mbunge huyo kabla ya kufanya mkutano mkubwa katika viwanja vya Seven Up Sinza Parestina. Mbunge Mnyika pia ametoa fedha taslimu sh. 100,000 …

Kikwete akiri nchi iko katika hali ya dharura

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watendaji wa Serikali yake kutambua kuwa nchi iko katika hali ya dharura kubwa ya upatikanaji wa nishati ya umeme, na hivyo wafanye maamuzi ya haraka, bila kigugumizi, kukabiliana na hali hiyo kwa manufaa ya wananchi. “Tuko katika hali ya dharura na mimi sioni hisia za uharaka wa kuchukua …

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TASWA Desemba 17, 2011

KAMATI ya Utendaji ya TASWA iliyokutana hivi karibuni, ilifikia uamuzi wa mkutano huo ufanyike eneo hilo lililopo Kilometa 37 kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kuwaweka pamoja kwa siku nzima waandishi wa habari za michezo na kubadilishana mawazo kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyotokea mwaka 2011. Nia ya TASWA ni kumaliza Mkutano Mkuu saa nane mchana …

Uzinduzi wa kinywaji Pilsner Lager cha SBL

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akigonganisha chupa kuashiria uzinduzi wa kinywaji aina ya Pilsner Lager na Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti Breweries Bi. Teddy Mapunda (kulia) na Mkurugenzi wa Masoko Bw. Ephraim Mafuru wa pili kutoka kushoto pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Pilsner Lager Maurice Njowoka kushoto.

Msanii Cabo Snoop wa Angola ndani ya Family Day

Mwanamuziki Cabo Snoop kutoka nchini Angola akifanya vitu vyake jukwaani huku akisasaidiwa na meneja wake kulia wakati wa tamasha la Family Day Bonanza lililofanyika jana kwenye viwanja vya Leadesr Kinondoni jijini Dar es salaam na kushirikisha pia wasanii kadhaa wa nyumbani Tanzania wakiwemo Diamond, Islay na Baendi ya African Stars ya jijini Dar es Salaam.