Wataalamu Tanzania waache kulalama- Jaji
*Asifu juhudi za Serikali kuleta maendeleo WAZIRI MKUU Mstaafu, Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba amesifu jitihada zilizofanywa na Serikali katika kuleta maendeleo nchini lakini amewaonya Watanzania waache tabia ya kulalamikia kila jambo na badala yake wafanye kazi. Ametoa kauli hiyo Oktoba 11, 2011 wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa na Ofisi ya …
Jaji Warioba ataka vyama vya siasa vijifunze kushindana
*Asema kila awamu ilikuwa na matatizo yake WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema vyama vya siasa nchini havina budi kujifunza kushindanisha sera na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyenyewe. Amesema hayo Jumanne, ya Oktoba 11, 2011 mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho …
Wanakijiji cha Mwanadilatu walalamikia uchimbaji mchanga
Na Joachim Mushi WANANCHI kutoka kijiji cha Mwanadilatu wamelalamikia kitendo cha uharibifu wa mazingira kinachofanywa na baadhi ya watu wanaochimba mchanga maeneo mbalimbali kijijini hapo. Wakizungumza na vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam kupitia kwa wawakilishi wa wananchi hao, Marko Nyaigana amesema kitendo cha kufanyika uharibifu wa mazingira eneo hilo kimepamba moto na sasa kinaharibu pia miundombinu. Mwakilishi …
Raia wa Liberia wajitokeza kupiga kura
RAIA wa Liberia jana wameshiriki katika uchaguzi wa pili tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo miaka minane iliopita. Shughuli ya kupiga kura inatarajiwa kuanza asubuhi hii ambapo wagombea kumi na tano wamejitokea kuwania kiti cha urais akiwemo rais wa sasa Ellen Johnson Sirleaf. Bi Sirleaf anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Winston Tubman wa chama cha …
Kauli ya UVCCM yaleta ‘utata’ CCM Arusha
Na Janeth Mushi, Arusha KAULI iliyotolewa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) imeibua mjadala baada ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, kuwataka UVCCM kutambua kuwa matatizo ya umoja huo hayawezi kupatiwa ufumbuzi nje ya chama hicho. Katibu huyo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoani Tanga ameongeza kwamba matatizo yoyote …