SBL yakabidhi vitabu vya sheria za usalama barabarani

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Teddy Mapunda (wa tatu kulia) akizungumza katika makabidhiano ya vitabu vya Sheria ya Usalama Barabarani katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Trafiki jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, na kulia ni Meneja wa Mahusiano wa (SBL), Nandi Mwiyombela, huku kushoto …

Polisi: Hatujazuia maandamano ya CCM Arusha

Na Janeth Mushi, Arusha POLISI mkoani Arusha wamekana taarifa zilizotolewa dhidi yao kuwa wamezuia maandamano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Oktoba 9 mwaka huu. Taarifa zilizoufikia mtandao huu zinadai kuwa Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha Abdallaha Mpokwa, ndiye aliyeomba kusitishwa kwa maandamano, wakati jeshi hilo likiwa tayari limeshatoa kibali …

Mapigano ya Wamasai, Wasonjo yazuka Ngorongoro

Na Janeth Mushi, Arusha BAADHI ya viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamelazimika kwenda eneo lililozuka mapigano baina ya Wasonjo na Wamasai kijijini Kisiwasuwi na Olorieni Magaidulu, Wilaya ya Ngorongoro kudhibiti ghasia na mapigano yaliozuka eneo hilo. Akizungumza leo mjini hapa Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo, Leonard Paul, amesema wameondoka arusha mchana huu kuelekea eneo hilo. Akitoa ufafanuzi zaidi …

JK awaachia huru polisi waliomuua Jenerali Kombe

WALIHUKUMIWA KUNYONGWA NA MAHAKAMA KUU, RUFAA Moshi ASKARI Polisi wawili waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe wameachiwa huru.Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku, ambao wamekuwa gerezani takriban kwa miaka 16, wamechiwa huru kwa huruma ya Rais Jakaya Kikwete …