Mtoto wa Kanali Gaddafi akamatwa

MTOTO wa Muammar Gaddafi aliyekuwa Rais wa Libya aliyeondolewa madarakani kwa nguvu za kijeshi, Muttasim Gaddafi ambaye alifanya kazi kama Mshauri Mkuu wa Usalama wa Kitaifa katika serikali ya babake amekamatwa. Ofisa mmoja wa Baraza la Mpito la Kitaifa nchini Libya (NTC) amesema Mutassim amekamatwa mjini Sirte na kupelekwa Benghazi japokuwa ofisa mwingine kutoka NTC amesema habari hizo bado hazijathibitishwa. …

Mama Salma Kikwete ataka wazee waenziwe

Na Anna Nkinda – Maelezo, Butiama JAMII nchini imetakiwa kutowadharau, kuwanyanyasa na kuwasahau wazee bali iwaenzi na kuwathamini kwani kupitia kwao itafaidika kwa kujifunza mambo mengi zaidi ambayo haikuwa inayafahamu. Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais wa kwanza na Muasisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Abeid Aman Karume Mama Fatma Karume wakati akiongea na wakazi wa …

Mama Kikwete awafunda wahudumu wa afya

Na Anna Nkinda – Butiama WAHUDUMU wa Afya nchini wametakiwa kufuata maadili yao ya kazi na kutoa kauli nzuri kwa wagonjwa ili kupunguza malalamiko yanayotolewa dhidi yao kutokana na utendaji wao mbaya wa kazi. Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wafanyakazi wa kituo cha Afya cha Butiama kilichopo wilayani Musoma katika Mkoa …

Mradi kabambe wa umeme kujengwa nchini

*Utagharimu mabilioni ya fedha *Utaunganisha mikoa yote kwenye Gridi ya Taifa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Oktoba 12, 2011, amepokea ripoti kutoka makampuni mawili ya kimataifa kuhusu Mpango Kabambe ya mradi mkubwa wa umeme ambao utaunganisha kwenye Gridi ya Taifa mikoa yote sita ambayo kwa sasa haiko kwenye gridi hiyo. Rais Kikwete …

Nape asema kuna wana-CCM wanaihujumu CCM

Na Mwandishi Wetu, KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kuna watu ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambao wamekuwa wakihujumu na kupotosha uamuzi wa chama hicho juu ya dhana ya kujivua gamba. Kiongozi huyo ametoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaa alipozungumza na vyombo vya habari. “Kumekuwepo na juhudi za muda mrefu …