Ole Sendeka asema CCM isisubiri kuwajibiswa na wananchi

Na Joachim Mushi MBUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Simanjiro, Christopher ole Sendeka amesema CCM isingoje kuwajibishwa na Wananchi bali ihakikishe inawang’oa mafisadi wote ndani ya chaa hicho ili kurudisha imani kwa wananchi na wanachama wake. Hata hivyo amesisitiza kuwa suala la kujivua gamba lisiishie ndani ya chama bali hadi serikalini. Sendeka ametoa kauli hiyo leo mjini hapa …

Mbio za Mwenge kuzindua miradi ya bil. 1.7 Arusha

Na Janeth Mushi, Arusha MIRADI 11 ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 1.7 ambayo imegharamiwa na Serikali Kuu, kwa kushirikiana na halmashauri, wahisani pamoja na wananchi inatarajiwa kuzinduliwa katika mbio za mwenge wa Uhuru. Aidha mwenge huo uliowashwa Kijijini Butiama mkoani Mara jana kwa lengo la kumuenzi Baba wa taifa Hayati Nyerere ambapo utazimwa Disemba 9 mwaka …

Kumbukizi ya miaka 12 ya kifo cha Nyerere

LEO Watanzania wanaadhimisha miaka 12 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyefariki tarehe kama ya leo mwaka 1999. Nyerere ambaye alikuwa muhimili wa Taifa la Tanzania alifariki Oktoba 14, 1999 katika hospitali ya St. Thomas ya London, Uingereza. Kiongozi huyu atakumbukwa milele kutokana na uadilifu, msimamo kimaamuzi, ujasiri na uwezo mkubwa wa uongozi aliokuwa nao wakati wa …

Polisi wasaka madaktari waliotekwa Kenya

POLISI wakitumia helikopta na magari wanawasaka watu wenye silaha waliowateka nyara madaktari wawili wa Uhispania wanaofanya kazi na shirika la misaada la Medicins Sans Frontiers (MSF) karibu na mpaka na Somalia nchini Kenya. Wawili hao walitekwa katika kambi ya wakimbizi ya Daadab, ambayo inawahifadhi maelfu ya wakimbizi wanaokimbia njaa katika Pembe ya Afrika. Taarifa zinazohusianasomalia, kenya, ulaya Dereva wao, raia …

Kikwete ashiriki mazishi ya Mwanahabari Penza

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Oktoba 13, 2011 aliungana na waombolezaji kumzika mwanahabari mkongwe, Juma Fugame Penza katika makaburi ya Kisutu, mjini Dar es Salaam. Ndugu Juma Penza alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kwenye Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 63. Marehemu Penza ambaye amekuwa katika tasnia ya habari …