Ikulu yakanusha JK kutoa msamaa wa vifo

*Ni kwa wanaodaiwa kumuua Lut. Generali Kombe Na Mwandishi Wetu GAZETI la Mwananchi, matoleo ya Jumatano, Oktoba 12 na Oktoba 13, 2011, limeandika habari zilizodai kuwa Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete alitoa msamaha wa kupunguza adhabu ya kifo iliyowakabili askari polisi wa zamani waliopatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumwua kwa makusudi aliyepata kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya …

Iran yaipa Tanzania power tiller 100

Na Mwandishi Maalum IRAN imetoa matrekta madogo aina ya power tiller 100 kwa Serikali ya Muungano wa Tanzania kusaidia kuinua na kuimarisha kilimo nchini na hasa kuunga mkono malengo ya Mpango wa Kilimo Kwanza. Mchango huo mkubwa wa kusaidia kuinua na kuboresha kilimo cha Tanzania umeelezwa na Balozi wa Iran katika Tanzania, Mheshimiwa Mohsen Movahhedi Ghumi kwa Rais wa Jamhuri …

Polisi yamsaka ‘bosi’ wa UVCCM Arusha

Na Mwandishi Wetu, Arusha JESHI la Polisi mkoani Arusha linamsaka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoani hapa, James Ole Millya kufuatia kauli aliyotoa kuwa Polisi imezuia maandamano ya CCM yaliyokuwa yafanyike Oktoba 9 mwaka huu jambo ambalo si kweli. Juzi polisi mkoani hapa ilikanusha madai ya kuzuia maandamano hayo na kuongeza kwamba CCM ndiyo walioandika barua na …

Mafisadi wamtisha Rais Kikwete, CCM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema ndani yake kuna kikundi cha waasi chenye nguvu ya pesa ambacho kinasaidia kuupa nguvu upinzani na kuandaa mkakati wa kutenganisha cheo cha urais na uenyekiti wa taifa wa chama. Kulingana na utaratibu CCM iliojiwekea, Rais anayekuwa madarakani ndiye anakuwa mwenyekiti wa chama hicho, hatua inayompa nguvu za kuongoza chama hicho kama sehemu ya dola. Katibu …