Katika ligi ya Ungereza West Bromwich Albion katika mchezo ulioanza mapema imefanikiwa kuzoa pointi tatu baada ya kuilaza Wolves mabao 2-0 na kufanikiwa kupata ushindi wa kwanza wa nyumbani na kujikwamu eneo la kushuka daraja. Chris Brunt alikuwa wa kwanza kuipatia West Brom bao la kuongoza baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Billy Jones. Kevin Doyle naye alikaribia kuipatia bao …
Arsenal yaikomalia Sunderland kwa 2-1.
Mabao mawili mazuri aliyofunga Robin van Persie yameiwezesha Arsenal kupata ushindi dhidi ya Sunderland katika uwanja wa Emirates. Nahodha huyo wa Arsenal alifunga bao la kwanza katika sekunde ya 29 tangu mchezo ulipoanza, bao linaloonekana ni la mapema sana kufungwa katika Ligi Kuu ya England msimu huu. Lakini ilionekana kama Sunderland ingepata pointi katika mchezo huo baada ya mchezaji wa …
Nape ‘avamia’ ngome ya Chadema
AZOMEWA, GREEN GUARD WATEMBEZA KIPIGO Mwanza MKUTANO wa hadhara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (pichani) uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Magoneni, Kirumba jijini hapa, uliingia dosari baada ya kundi la vijana kuwazomea viongozi karibu wote wa chama hicho waliopanda jukwaani na kukifanya kikundi cha ulinzi cha CCM, Green Guard kutembeza kipigo hadharani.Katika mkutano huo, Nape …
Pinda ataka uwekezaji uwanufaishe wananchi
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema wakati Serikali inapiga mbiu ya uwekezaji, itahakikisha kuwa uwezekezaji mkubwa unaofanyika katika kilimo unawanufaisha wakulima wadogo ambao wanazunguka maeneo watakayopewa wawekezaji. Ametoa kauli hiyo jana Jumapili, Oktoba 16, 2011 wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua mabanda ya maonesho nje ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ambako Mkutano Mkubwa wa …
Vodacom yashiriki Mkutano wa Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika
Na Mwandishi Wetu, Mpanda KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Vodacom inashiriki Mkutano wa Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika ulioanza jana mjini Mpanda kwa maonesho ya bidhaa na huduma kutoka wadau anuai wa uwekezaji nchini. Akitoa maelezo ya huduma na bidhaa za Vodacom kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyetembelea banda la Vodacom katika maonesho hayo, Meneja Mawasiliano wa Vodacom, …