Millya aandamana na UVCCM kwenda Polisi
Na Janeth Mushi, Arusha VIJANA wa Jumiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoani hapa, jana wameandamana hadi Kituo Kikuu cha Polisi kumsindikiza Mwenyekiti wa Umoja huo mkoani hapa, James Ole Millya ambaye alitakiwa kujisalimisha kwa Jeshi la polisi ili athibitishe kauli aliyoitoa dhidi ya jeshi hilo wakati wa mkutano ulioambatana na kuzinduliwa kwa matawi wilayani Arusha. Aidha vijana …
Kesi ya kupinga ubunge wa Lema yakwama tena
Na Janeth Mushi, Arusha KESI ya kupinga matokeo ya ubunge wa Godbless Lema (CHADEMA) Jimbo la Arusha Mjini, imekwama kuanza usikilizwaji wa awali tena hadi Jumatatu ijayo baada ya mahakama hiyo kushindwa kuwasilisha nyaraka muhimu, zilizokuwa zinahitajika kwa mawakili wa upande wa wadaiwa. Kesi hiyo inayosikilizwa katika mahakama kuu Kanda ya Arusha, Jaji anayesikiliza kesi hiyo Aloyce Mjulizi, akiahirihsa kesi …
APRM kueleza mafanikio, changamoto za utawala bora Zanzibar
Na Hassan Abbas MPANGO wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) utawaeleza viongozi mbalimbali wa kisiasa na watendaji wengine Zanzibar juu ya mafanikio katika kujenga misingi ya utawala bora nchini katika miaka 50 ya uhuru na changmoto zake. Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania, Rehema Twalib mpango huo umeandaa semina mbili kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Makatibu …
Al-Shabbaab kukabiliana na majeshi ya Kenya- Somalia
Wanamgambo wa Al-Shabaab nchini Somalia wameahidi kulipiza kisasi dhidi ya wanajeshi wa Kenya walioingia katika ardhi ya Somalia kwa lengo la kuwatafuta raia wanne wa Ulaya waliotekwa nyara wiki iliyopita. Wanajeshi wa Kenya walivuuka mpaka na kuingia katika ardhi ya Somalia kiasi kilomita 100 kutoka eneo la mpaka wa kaskazini mwa Kenya hapo jana (16.10.2011), wakisaidiwa na helikopta. Hatua hiyo …
Vuguvugu la “occupy” linasambaa
Maandamano duniani kote ya kupinga kile waandamanaji wanakiona kama uroho na usimamizi mbaya wa uchumi duniani yameingia siku ya pili. Katika miji kadhaa – kutoka Auckland hadi Toronto – waandamanaji walikesha katika mahema kushinikiza wanasiasa wachukue hatua. Haijawa wazi iwapo maandamano yanaanza kushikamana na kuwa kitu kikubwa. Mjini London, msemaji alisema lengo ni kuiga mambo yanayotokea mjini New York, katika …