WAFUNGWA wapatao 295 wa Palestina wataachiwa kati ya kundi la 477 waliorodheshwa. Shughuli hiyo inatazamiwa kuendelea kwa muda wa saa kadhaa. Magari ya kwanza ya msafara huo yatakayowasafirisha wafungwa wa kike tayari yameondoka kwenye jela moja yakielekea eneo la Ukingo wa Magharibi. Maofisa wa Usalama wa Misri, iliyousimamia mchakato huo wa kufikia makubaliano ya kubadilishana wafungwa, ndio wanaousindikiza msafara huo. …
Wenger hana hofu mkataba wa Van Persie
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hana wasiwasi kwamba Robin van Persie si mwenye haraka ya kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo. Nahodha wa Arsenal, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2013, amesisitiza “nafsi yake imejitolea kwa klabu ya Arsenal”. Wenger amesema: “Iwapo utakuwa umejiwekea asilimia 100 hadi siku ya mwisho ya mkataba wako, hiyo yote naiita ni kujifunga kabisa. “Kwangu …
Al-shabab kulipiza kisasi, kuipiga Kenya
MSEMAJI wa kundi la wapiganaji wa Al-Shabab, Sheikh Ali Dheere amesema wako tayari kulipiza kisasi kwa kuyashambulia majengo ya Kenya na kuzorotesha uchumi wa nchi hiyo. Akizungumza na Idhaa ya Kisomali ya BBC, Sheikh Dheere amenukuliwa akisema; “Tunaiambia serikali ya Kenya na watu wake kuwa wametangaza vita, hawajui vita ni nini, ni kubomoa majengo ya orofa na yanayopendeza nchini Kenya …
Mwanajeshi wa Israeli kuachiliwa huru
MWANAJESHI mmoja wa Israeli Gilad Shalit, anatarajiwa kuachiliwa huru leo, baada ya kuzuiliwa kwa miaka mitano, huku wafungwa wa Palestina wapatao 1,000 wakiachiliwa huru kufuatia makubaliano na kundi la Hamas. Shalit mwenye umri wa miaka 25, alitekwa nyara mwaka wa 2006 na wanamgambo wa Hamas ambao walipitia njia za chini ya ardhini kuingia Israeli kutoka Gaza. Hapo jana mahakama ya …
Wafuasi wa Gaddafi waingia Mali
Wapiganaji wa kabila la Tuareg waliorudi Mali kutoka Libya wanaaminika kusaidia katika kuanzisha kundi jipya la waasi. Kundi hilo la National Movement for the Liberation la Azawad NMLA limesema ni matokeo ya muungano baina ya makundi mawili ya waasi, yaliyoongezwa nguvu na Watuareg waliopigana kwa ajili ya Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya. Watuareg wa Mali wamelalamika kwa muda mrefu kwa …
SMZ yapanga kufanya mageuzi ya kilimo
Na Rajab Mkasaba Ikulu, Zanzibar MTAZAMO wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kufanya mageuzi makubwa ya kilimo kwa kutumia nyenzo bora, mbolea na utaalamu na kufikia uzalishaji wa chakula hadi kuweza kuuza ziada ya chakula hicho kwa lengo la kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo …