CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kinasikitika kutangaza kifo cha mwandishi mahiri wa habari za michezo Zanzibar, Maulid Hamad Maulid. Maulid ambaye anafanyia kazi vituo vya Redio One na ITV akiwa Zanzibar, amefariki dunia leo Jumanne Oktoba 18, 2011 asubuhi nyumbani kwake Jang’ombe Zanzibar. Taswa imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Maulid kwani alikuwa kiungo …
Pinda ataka halmashauri zitenge maeneo ya Benki ya Ardhi
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kutenga maeneo maalum kwa ajili ya uwekezaji ili baadaye yatumike kama land bank (akiba ya ardhi) kwa urahisi. Amesema watendaji wa Halmashauri wakishatenga maeneo hayo, hawana budi kuwasiliana na Mamlaka ya Kuendeleza Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) ili wanapojitokeza wawekezaji maeneo hayo yawe yamekidhi vigezo vinavyohitajika. Ametoa kauli hiyo Oktoba 17, …
T-Moto kuanza kuwasha moto mkoani Mtwara
*Kutoa msaada wa kitanda cha wajawazito Hospitali ya Mkoa Mtwara KUNDI jipya la taarab linalokuja kwa kasi nchini, Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ama ‘Real Madrid’ linatarajia kuanza kufanya maonyesho mawili katika mkoa wa mtwara. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa mara tu baada ya uzinduzi wa kundi hilo unaotarajia kufanyika Oktoba 28, …
Rais Kikwete amteua Balozi Kazaura Mkuu wa Chuo UDSM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Fulgence Kazaura kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kipindi kingine cha miaka minne. Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Oktoba 18, 2011, na Katibu Mkuu Kiongozi Phillemon Luhanjo imesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja leo hii. Balozi Kazaura alikuwa Mkuu wa Chuo hicho …
Balozi Amina Ali atunukiwa tuzo ya Mwanadiplomasia wa mwaka
Mwandishi Maalum BALOZI wa Umoja wa Afrika nchini Marekani Bi. Amina Salum Ali ametunukiwa tuzo ya Mwanadiplomasia wa Mwaka na Taasisi ya Jumuiya za Africa jimbo la Michigan nchini Marekani. Balozi Ali alitunukiwa tuzo hiyo katika sherehe kubwa iliyoandaliwa na Muungano wa Jumuiya za Waafrika kwenye jimbo hilo iliyofanyika katika jiji la Detroit nchini Marekani usiku wa Oktoba, 2011. Balozi …
Saudi Arabia kuwasilisha malalamiko Baraza la Usalama
UONGOZI wa Saudi Arabia unataka kuyawasilisha katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, malalamiko baada ya kubainika njama ya kumuua balozi wake nchini Marekani. Inadaiwa kuwa Iran ilihusika na upangaji wa njama hiyo. Hata hivyo, kwa mujibu wa balozi wa Saudi Arabia katika Umoja wa Mataifa, inachokitaka serikali yake bado hakijakuwa bayana. Kwa upande wa, Baraza la Usalama la …