Wananchi watakiwa kusimamia kesi za ukatili zifike mahakamani
Na Ananilea Nkya Mkurugenzi Mtendaji TAMWA. WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wameshauriwa kusimamia kesi zao zinazohusu ukatili wa kijinsia kuhakikisha zinafikishwa katika vyombo vya sheria. Mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai, mkoa wa Kusini Unguja SSP Makaran Khamis Ahmed amesema kesi nyingi za ukatili hazifikishwi Mahakamani kutokana na wananchi kuanzisha tabia ya kuhukumu kesi katika ngazi za shehia, …
Semina ya Jinsia na Maendeleo
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) unawakaribisha wananchi wote katika mfululizo wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) zinazofanyika kila Jumatano. Wiki hii itakuwa ya POLICE JAMII/ TPFnet WATAWASILISHA: MADA: DHANA YA POLISI JAMII KATIKA KULINDA USALAMA NA AMANI NCHINI Siku ni: Jumatano Tarehe 19 Oktoba, 2011 na Muda: ni Saa 09:00 – 11:00 Alasiri. MAHALI: Viwanja vya TGNP, Barabara ya …
Kila binadamu ‘anakichaa’ chake bwana!
KAMERA ya dev.kisakuzi.com leo imelinasa tukio hili katika barabara ya Morogoro karibu na Jengo la Ubungo Plazza. Mtu huyu pichani kwa kipindi kirefu amekuwa akionekana kukusanya mabaki ya vifaa vya magari na kutengeneza makazi yake pembezoni mwa barabara hio. Eneo hili ndilo mtu huyu amefanya kama makazi yake na muda mwingi huutumia kuendelea kuikarabati (kuiboresha) kila anapokuwa eneo hilo na …
Israel, Palestina washerehekea kubadilishana wafungwa
MAKUNDI ya watu wenye furaha nchini Israel na Palestina wamekuwa wakisheherekea mpango wa kihistoria wa kubadilishana wafungwa. Israel iliwaachiliwa huru mamia ya wafungwa wa Kipalestina, ikiruhusu wengi wao kurudi katika eneo la Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan, na badala yake kukabidhiwa askari wa Kiisrael Gilad Shalit. Sajini Shalit aliyekuwa amezuiliwa katika eneo la Gaza kwa zaidi ya …
Chanjo ya malaria yatoa matumaini
MAJARIBIO ya chanjo ya malaria barani Afrika yametoa matumaini ya kupatikana kwa chanjo ya kwanza diniani ya ugonjwa huo, unaoenezwa na mbu. Watoto waliopata chanjo hiyo ya majaribio wana nafasi nusu ya kupata ugonjwa huo. Zaidi ya watoto 15,000 chini ya miezi kumi na minane walihusishwa katika utafiti huo uliochapishwa katika jarida linalojadili maswala ya kimatibabu la New England Journal …