Na Anna Nkinda – Maelezo WATANZANIA wametakiwa kujenga tabia ya kujitolea kufanya kazi kwa moyo na kushiriki katika shughuli za kujiongezea kipato kwa lengo la kujikwamua kimaisha, kwani hakuna mafanikio yatakayopatikana bila ya kufanya kazi kwa bidii. Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akizindua Umoja wa Vikundi vya kuweka Akiba na Kukopa vilivyopo chini …
Waandaji wa “Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge” watangaza njia
*Ni zile zitakazotumika kwenye mashindano hayo VODACOM Tanzania ambao ni waandaaji wa mbio za baiskeli zijulikanazo kama “Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge” wametangaza njia (route) zitakazotumika kwenye mashindano ya baiskeli ambazo zitaanzia mjini Shinyanga na kumalizikia jijini Mwanza Oktoba 22 yanayotarajia kugharimu zaidi ya sh. milioni 50. Akizungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Mwanza leo, katika ofisi ya Vodacom Kanda …
Uingereza yaionya Algeria
WAZIRI wa mambo ya nje wa Uingereza , William Hague, ameitaka Algeria iheshimu sheria ya kimataifa kwa kuwakabidhi watoro wa vita nchini Libya. Mke wa Kanali Gaddafi na wanawe watatu walivuka mpaka wa Algeria wakikimbia mapambano nchini Libya mnamo mwezi wa Agosti. Akiongea baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Bwana Hague aliwaonya viongozi wa Algeria …
Kenya na harakati za kiusalama
KENYA inapanga kuanzisha harakati za kiusalama ndani ya nchi dhidi ya washirika wa kundi la wapiganaji wa Al Shabaab. Kulingana na naibu waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya Kenya, Orwa Ojodeh, harakati hizo zitakuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa na zitafanyika mjini Nairobi. Maeneo yatakayolegwa ni kama vile mtaa wa Eastleigh ulioko Mashariki mwa mji huo, ambako raia wengi …
Lowassa: Uvumilivu sasa basi
Monduli WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amevunja ukimya na kuzungumzia tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake, huku akisisitiza kuwa sasa amechoka kukashifiwa. Alisema kuanzia sasa hatakubali kuchafuliwa jina lake na mtu yeyote au chombo chochote cha habari na atakayefanya hivyo, ajiandae kukabiliana na mkono wa sheria. Lowassa alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake katika Kijiji cha …
Ujenzi wa Kituo cha Wanafunzi UDSM ni msaada kwa wanafunzi- JK
Na Mwandishi Wetu RAIS wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema kuwepo kwa Kituo cha Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kutakidhi mahitaji mengi mbalimbali ya wanafunzi hasa wale wanaokaa nje ya chuo hicho. Rais Kikwete ametoa kauli hiyo jana Dar es Salaam alipokuwa kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha wanafunzi katika chuo cha UDSM. Akizungumza kwenye …