AU yakana ‘propaganda’ za Somalia
UMOJA wa Afrika umekataa kwamba miili ya watu 70 iliyoonyeshwa na wapiganaji wa Kisomali wa kundi la al-Shabab ni askari wa umoja huo waliouawa kwenye mapigano. Al-Shabab iliwaonyesha waandishi wa habari miili hiyo, wakidai askari wa Burundi waliuawa Mogadishu siku ya Alhamisi. Msemaji wa Umoja wa Afrika AU amekana madai hayo na kusema ni propaganda na kusema askari wake 10 …
ICC yaihoji Malawi kuhusu Rais Bashir
MAHAKAMA ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imeitaka Malawi kueleza kwanini ilishindwa kumkamata Rais wa Sudan Omar al-Bashir katika ziara yake ya hivi karibuni. ICC imetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Bw Bashir kwa mashtaka ya mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita wakati wa mgogoro huko Darfur. Malawi ni moja ya nchi zilizotia saini makubaliano ya kuridhia …
Mazishi ya siri ya Gaddafi
MAMLAKA nchini Libya zinafanya mipango ya kufanya mazishi ya siri kwa kiongozi aliyeondolewa madarakani Kanali Muammar Gaddafi, baada ya kukamatwa na kuawa, BBC inafahamu. Hata hivyo, inaonekana huenda kukawa na kuchelewa kufayika kwa mazishi hayo, ambayo chini ya utamaduni wa Kiislam mazishi hufanyika haraka iwezekanavyo. Waziri wa mafuta Ali Tarhouni ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa mwili wa Kanali …
India yaitandika England katika kriketi
India ikicheza nyumbani iliicharaza England 3-0 nakupata ushindi wa wiketi tano. Ikijitahidi ifanikiwe kupata runs 299, ilianza vyema kupitia wachezaji Ajinkya Rahane, aliyefanikiwa kupata runs 91, lakini harakaharaka ilipoteza wiketi nne, lakini bado kufanikiwa kuonyesha ustadi mwishomwisho wa mchezo. Mahendra Dhoni, pasipo kuondolewa, aliweza kuiletea timu yake ushindi kwa kupata runs 35. Hapo awali, Jonathan Trott, bila kuondolewa, aliisaidia England …
Kalou ataka nafasi zaidi Chelsea
SALOMON Kalou, mchezaji wa Ivory Coast ambaye huichezea Chelsea, ameielezea klabu hiyo kupata hakikisho kwamba atacheza mechi zaidi, kabla ya kukubali kutia saini mkataba mpya Stamford Bridge. Kalou, mwenye umri wa miaka 26, ameamua kuondoka katika klabu hiyo mara mkataba wake utakapokwisha msimu huu, kwani anakerwa kwa kutocheza mechi kila wikendi Naye Meneja Andre Villas-Boas alifichua wiki iliyopita kwamba majadiliano …