Ndege yaanguka Arusha yaua na kujeruhi

Na Mwandishi Wetu, Arusha NDEGE ndogo ikiwa na marubani wawili imeanguka na kusababisha kifo cha mmoja wao huku mwingine akijeruhiwa vibaya. Rubani aliyepoteza maisha katika ajali hiyo ni Ally Harun (24) na mwenzake, Liliani Koima akijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya rufaa ya KCMC, mkoani Kilimanjaro Moshi. Ndege hiyo yenye usajili namba 5H/QTE mali ya kampuni ya World Quality Travel …

Kariakoo kwatapakaa maji ya mavi!

Na Mwandishi Wetu MAENEO kadhaa ya Soko la Kimataifa la Kariakoo ambalo ni maarufu jijini Dar es Salaam leo tangu majira ya asubuhi yalikuwa yametapakaa maji ya vinyesi yaliyokuwa yakitoka katika njia ya maji machafu. Mwandishi wa habari hizi aliyekuwa eneo la tukio ameshuhudia maji hayo yakitoka kwenye baadhi ya chemba za vyoo na kutiririka hovyo, hali iliyokuwa kero kwa …

NATO kusitisha mashambulio Libya wiki ijayo

JUMUIYA ya NATO imesema ina mpango wa kusitisha ujumbe wa kijeshi wa kushambulia maeneo nchini Libya yaliyodumu miezi saba, ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, siku moja baada ya kuuwawa Muammar Gaddafi. NATO ina mpango wa kusitisha mashambulio yake ya anga na baharini yaliyodumu miezi saba chini Libya, ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, siku moja baada ya kifo cha kiongozi wa …

Mzozo wazuka kuhusu mazishi ya Gaddafi

MAZISHI ya Kanali Gaddafi yamesitishwa kutokana na tofauti zilizozuka baina ya maofisa wa Libya kuhusu jinsi ya kufanya maziko hayo. Chini ya utamaduni wa Kiislam, maziko hutakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo. Lakini Waziri wa Mafuta wa Libya amesema mwili wa Gaddafi huenda ukahifadhiwa kwa siku kadhaa. Taarifa kutoka Libya, barani Afrika zinasema haijafahamika kama kiongozi huyo wa zamani atazikwa mjini Sirte, …

Waandishi wapatiwa mafunzo namna ya kuripoti ukatili

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana kimetoa mafunzo kwa wanahabari zaidi ya 30, ambao wanaandaliwa kwa lengo la kuripoti habari za unyanyasaji wa kijinsia (GBV) hapo baadae katika baadhi ya mikoa. Wanahabari hao wamepata mafunzo hayo ikiwa ni hatua ya kuandaa kundi maalumu la wanahabari ambalo litakuwa likiripoti kwa kina habari dhidi ya vitendo vya kikatili kwa wanawake …