Prince wa Saudi Arabia afariki Dunia

Prince Sultan ambaye angeweza kurithi ufalme, alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 80, na amekuwa akitibiwa saratani nchini Marekani. Prince Sultan alikuwa mtoto wa mwanzilishi wa taifa la Saudi Arabia, Ibn Saud, na ni baba mmoja na mfalme wa sasa, Abdullah, ambaye piya ana zaidi ya miaka 80. Mwandishi wa BBC Mashariki ya Kati anasema inavoelekea mtoto mwengine mwanamume …

Maiti ya Gaddafi yakaguliwa Mjini Misrata

OFISA anayechunguza vifo vya ghafla nchini Libya anakagua mwili wa Kanali Muammar Gaddafi leo, huku bado idadi kubwa ya watu ulimwenguni wakihoji namna kiongozi huyo alivyo uwawa. Taarifa kutoka nchini Libya zinaeleza kwa sasa maiti ya Gaddafi iko katika chumba cha barafu (jokofu) cha kuweka nyama mjini Misrata – ikiwa na alama ya risasi kichwani. Familia ya Kanali Gaddafi inataka …

China kuanzisha upasuaji wa kisasa Zanzibar

Na Rajab Mkasaba, Ikulu-Zanzibar UJUMBE kutoka Jimbo la Jiangsu nchini China umesema utaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika uimarishaji wa sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kuanzisha upasuaji kwa njia za kisasa na mradi wa tabasamu kwa kuwafanyia upasuaji watoto wanaozaliwa na athari za midomo. Ujumbe huo umeeleza hayo leo Ikulu mjini Zanzibar, wakati ulipokuwa na mazungumzo na Rais wa …

Makubaliano ya Kongamano la Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika

HIVI karibuni wilayani Mpanda lilifanyika Kongamano la Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika (Oktoba 17, 2011) na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 300. Mgeni rasmi katika Kongamano hilo alikuwa ni Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda (MB) alikuwa ni Mwenyekiti wa Kongamano hilo. Kongamano lilihudhuriwa na mawaziri mbalimbali, mabalozi, wawekezaji kutoka ndani na nje ya …

Wananchi: Tafiti za utawala bora za APRM zifanyiwe kazi

Na Mwandishi Wetu Wananchi wa kada mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali jijini Dar es Salaam wamesema katika kuboresha na kuinua utawala bora nchini miaka 50 ijayo ni vyema Serikali ikafanyiakazi tafiti mbalimbali zinazofanywa na taasisi zake hasa tafiti za utawala bora zinazofanywa na APRM. Wananchi hao walitoa maoni hayo kwa nyakati tofauti walipotembelea banda la Wizara ya Mambo …