TETEMEKO la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 7.3 cha Richter mashariki mwa Uturuki leo limeua kati ya watu 500 hadi elfu moja. Profesa, Mustafa Erdik Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Matetemeko ya Ardhi ya Kandilli mjini Istanbul ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba watu 500 hadi 1,000 wanakadiriwa kuwa wameuwawa katika tetemeko hilo. Kwa mujibu wa maafisa …
Man United chali, yapigwa 6-1 kwao
MANCHESTER City imeizaba Manchester United 6-1 kwenye uwanja wa Old Trafford. Kinyume na matarajio ya Wengi, Man United walishindwa kabisa kuhimili vishindo vya majirani zao na mahasimu wao wa jadi. Hadi mapumziko City walikuwa wakiongoza kwa goli moja lililofungwa na Mario Balotelli. Man United walicheza karibu kipindi chote cha pili wakiwa na mchezaji mmoja pungufu baada ya beki, Jonny Evans …
Chelsea nayo hola kwa QPR
Chelsea imebanwa na QPR na kuchapwa 1-0 katika mchezo uliojaa vuta nikuvute na kadi nyingi. Bao hilo pekee la QPR limefungwa na Heidar Helgoson katika dakika ya 10 kwa mkwaju wa penati. Penati hiyo ilitokana na Helguson kusukumwa ndani ya boksi na David Luiz. Jose Bosingwa alioneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Shaun Wrght Phillips, kabla ya Didier Drogba naye …
Watu 13 wajeruhiwa shambulio mjini Nairobi
SHAMBULIO la guruneti katika Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi, limesababisha watu 13 kujeruhiwa huku mmoja kati yao kujeruhiwa vibaya kufuatia shambulio hilo. Taarifa za awali zinasema guruneti hilo limerushwa na mtu asiyejulikana. Taarifa zinaeleza kuwa mtu huyo alifika kwenye eneo la burudani na baada ya mlango kufunguliwa alirusha guruneti na kukimbia. ”Mwanamume mmoja aligonga mlango akijifanya kama mteja na aliporuhusiwa …
Odinga: Kenya kuandaa Kombe la Dunia
WAZIRI Mkuu wa Kenya amesema nchi hiyo inaweza kuandaa mashindano ya kandanda ya Kombe la Dunia hivi karibuni. Taarifa zinasema, Raila Odinga anataka nchi hiyo kuwa mwenyeji wa mashindano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 kabla haijajaribu kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia. “Tutawekeza fedha zaidi siku zijazo katika kandanda nchi kwetu. Kusema kweli tunataka kujitokeza …
Uchaguzi huru wafanywa Tunisia
WANANCHI wa Tunisia wanapiga kura leo kuchagua bunge litalotayarisha katiba mpya na kumteua rais wa muda. Taarifa zinazohusianaAfrika, Siasa Tunisia ilikuwa ya mwanzo kuanza ghasia za mabadiliko katika nchi za Kiarabu baada ya kijana mmoja, Mohamed Bouazizi kujichoma moto, kupinga dhuluma za uongozi. Huu ndio uchaguzi wa mwanzo huru tangu Tunisia kupata uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka wa 1956, na …