Gaddafi kuzikwa leo jangwani kwa siri

BARAZA la Mpito la Libya limearifu kuwa Muammar Gaddafi atazikwa jangwani leo katika sehemu ya siri. Mwakilishi mmoja wa Baraza hilo ambae hakutaka kutajwa ameleeza hayo na kuongeza kuwa Gaddafi atazikwa pamoja na mwanawe Mutassim. Habari zaidi zinasema kwamba ilishindikana kufikia makubaliano juu ya kuukabidhi mwili wa Gaddafi kwa watu wa kabila lake. Hapo awali Baraza la Mpito lilihakikisha juu …

Chama cha kiislamu chajitangazia ushindi Tunisia

CHAMA cha kiislamu chenye msimamo wa wastani nchini Tunisia, Ennahda, kimejitangazia ushindi katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo. Matokeo rasmi yanatarajiwa baadaye siku ya Jumanne, lakini matokeo ya awali yanaonyesha kuwa chama cha Ennahda kitapata kura nyingi zaidi. Wapinzani wao wakuu, chama kinachofuata mfumo usio wa kidini cha PDP, wamekubali kushindwa. Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wameupongeza uchaguzi …

Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Kenya Mathew Iteere akiongea na waandishi wa habari mjini Nairibi

Kenya yalipuliwa tena, mmoja auawa 11 wajeruhiwa

TAARIFA kutoka Kenya zinasema kumetokea mlipuko mwingine katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Nairobi. Polisi wanasema mtu mmoja ameuawa na wengine kumi na wawili wamejeruhiwa. Mlipuko huo umetokea kwenye kituo cha basi. Kamishna wa Polisi Mathew Iteere amesema shambulio hilo halina uhusiano na shambulio lilitokea kwenye baa Jumatatu. Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu,”majeruhi wanane wamekimbizwa hospital ya Taifa …

Mnyika kuwasilisha muswada wa kudhibiti bei ya bidhaa muhimu

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), amesema kuwa atapeleka muswada binafsi wa Sheria ya Udhibiti wa Bei ya bidhaa nchini katika Mkutano ujao wa Bunge unaotarajiwa kuanza Novemba, mwaka huu kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu kasi kubwa ya mfumuko wa bei ya bidhaa. Mnyika alisema asilimia 70 ya wananchi wanalalamikia mfumuko wa bei ya …

Maalim Seif: Watendaji Zanzibar chanzo cha uchafuzi wa mazingira

Na Mwinyi Sadallah Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema tabia ya watendaji kufungia sheria na kanuni za uhifadhi wa mazingira katika makabati, ndiyo chanzo cha kuenea kwa uchafuzi wa mazingira visiwani humo. Maalim Seif, alisema sababu za uchafuzi wa mazingira Zanzibar sio ukosefu wa sheria na kanuni, bali sheria hizo hazitekelezwi na watendaji kwa kuhofia …

Jaji akwamisha kesi ya Lema kusikilizwa

Na Mwandishi Wetu, Arusha KESI ya kupinga matokeo ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA) leo imekwama kusikilizwa tena baada ya Jaji anayesikiliza shauri hilo, Aloyce Mujulizi kupata dharura na kuahirishwa kesi hiyo hadi Oktoba 27, 2011. Kwa mujibu wa Msajili wa Wilaya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, George Heberta ambaye alitoa taarifa ya dharura yaani safari …