Na Joachim Mushi KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemuengu Michael Wambura kugombea nafasi ya uenyekiti katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu mkoani Mara (FAM). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratius Lyatto imesema imeliondoa jina la Wambura kwa kile kukosa sifa ya …
Finland kuendeleza mradi wa mazingira Zanzibar
Na Rajab Mkasaba, Ikulu- Zanzibar FINLAND imesema itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza mradi wa kutunza mazingira hapa Zanzibar (SMOLE). Balozi wa Finland nchini Tanzania Sinikka Antila aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungunzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar. …
Dk. Bilal aiwakilisha Tanzania Mkutano wa Mawasiliano Kimataifa
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa ITU (International Telecommunication Union) unaohusu wajibu nchi katika dhana ya mawasiliano unaofanyika jijini Geneva. Makamu wa Rais ambaye ameambatana na wadau wa masuala ya mawasiliano kutoka Tanzania, sambamba na kushiriki kutoa mada katika mjadala unaohusu ‘Utandawazi na Dunia kuwa kijiji’ mjadala ambao …
Mechi ya Kagera Sugar Vs Coastal yasogezwa mbele
MECHI namba 89 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Kagera Sugar na Coastal Union iliyopangwa kufanyika Novemba 2 mwaka Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba imesogezwa mbele kwa siku moja. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia Ofisa Habari wake, Boniface Wambura imesema uamuzi wa kusogeza mechi hiyo hadi Novemba 3 mwaka …
TFF yawataja viingilio na waamuzi mechi ya Simba na Yanga
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetaja wamuzi watakao kuwa na kibarua cha kuchezesha mechi namba 78 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu za Yanga na Simba itakayofanyika Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika taarifa ya TFF iliyotolewa na Ofisa Habari wake leo, Boniface Wambura imemtaja mwamuzi wa Shirikisho …
Dk. Magufuli awakoromea Makandarasi
*Aanza utekelezaji ahadi ya ujenzi wa daraja Igunga Na Martin Ntemo, Habari- Wizara ya Ujenzi WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli (Mb), ametoa onyo kali kwa wakandarasi ambao wamesitisha kazi za ujenzi wa miradi ya barabara hasa ile ya maendeleo kwa kisingizio cha kutokamilishiwa kwa malipo ya awali. Magufuli aliyasema hayo hivi karibuni akiwa ziarani katika wilaya za Nzega …