Man U, Arsenal zasonga mbele Carling

Manchester United imesonga mbele na kuingia katika 16 za mwisho baada ya kuizaba Aldershot 3-0 katika mchezo wa raundi ya nne wa Kombe la Carling. Magoli ya United yalifungwa na Dimitar Berbatov, Michael Owen na Antonio Valencia. Arsenal nayo imeichapa Bolton 2-1. Bolton ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Gunners kupitia Fabrice Muamba. Hata hivyo Arsenal walijibu mashambulizi na …

Polisi wanasa maguruneti na bunduki-Kenya

MTU MMOJA amekamatwa na polisi na silaha mbali mbali katika mtaa mmoja mjini Nairobi,Kenya. Katika nyumba hiyo polisi walinasa maguruneti 13 na bunduki kadhaa pamoja na risasi. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi nchini Kenya Mathew Iteere, mtu aliyekamatwa anashukiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi. “Sina shaka kuwa tutapata habari muhimu kutoka kwake na kuweza kuwatia mbaroni wanachama wengine …

Jaji Mkuu Tanzania awania nafasi ya Ocampo

JAJI MKUU wa Tanzania Mohamed Chande Othman kuwania nafasi ya Ocampo ICC Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman ni mmoja kati ya watu wanne muhimu wanaoweza kushika nafasi ya Mwendesha Mashtaka katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa iliyoko The Hague, nchini Uholanzi. Nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Luis Moreno-Ocampo itakuwa wazi hapo mwakani baada ya Bw Ocampo …

Kanali Gaddafi mwanae wazikwa kisiri Libya

MAZISHI ya Kanali Muammar Gaddafi, mwanae Mutassim na Waziri wa Ulinzi yamefanyika katika sehemu ya siri leo alfajiri. Taarifa zilizotolewa na mmoja wa wasemaji wa Baraza la Kitaifa la Mpito (NTC) ameiambia BBC kuwa miili ya watu hao watatu imezikwa baada ya utata kuhusu kuvutana wapi wazikwe. Awali baadhi ya ndugu na jamaa wa kabila moja na Kanali Gaddafi waliomba …

Uhuru One kutoa laptop kwa wanafunzi Tanzania

Na Mwandishi Maalumu, Geneva, Switzerland KAMPUNI ya Uhuru One inaangalia uwezekano wa kutoa mafunzo ya matumizi rahisi ya kompyuta ndogo (laptop) mpango ambao utakwenda sambamba na kuwawezesha na kuwasambazia wanafunzi wa Tanzania ili waweze kuzitumia kompyuta hizo. Taarifa hiyo imetolewa le mjini Geneva, Switzerland na Meneja wa Uhuru One, Mihayo Wilmore, alipokuwa akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano …