Mama Zakhi Bilal mgeni rasmi uzinduzi wa T-Moto

MKE wa Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi wa kundi jipya la muziki wa taarab na albam ya kwanza ya kundi hilo (Tanzania Modern Taarab ‘T-Moto’ au Real Madrid), ambalo kwa sasa limekuwa gumzo kwa mashabiki wa muziki huo nchini. Akizungumza na mwandishi wa habari, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, …

MAPENDEKEZO JUU YA MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 2011

JUKWAA la Katiba Tanzania, linapenda kuwasilisha mapendekezo ya wananchi juu ya Muswada wa Sheria ya kuweka utaratibu wa mabadiliko ya Katiba Tanzania kama ifuatavyo. Maoni haya ni matokeo ya uchambuzi wa JUKWAA LA KATIBA TANZANIA wa maoni yaliyokusanywa kutoka kwa watanzania walioshiriki midahalo, semina, makongamano na mahojiano mbalimbali yaliyoandaliwa na JUKWAA LA KATIBA TANZANIA, asasi wanachama wake na makundi mengine …

Madeni Ulaya yawatatiza viongozi G8

VIONGOZI wa nchi tajiri, G20 wanakutana nchini Ufaransa wakiwa na hofu kuu kuhusu athari za mzozo wa madeni barani Ulaya kwa uchumi wa dunia. Mkutano huo unafanyika siku moja baada ya viongozi wa umoja wa ulaya kusimamisha misaada ya euro bil. 8 kwa Serikali ya Ugiriki hadi matokeo ya kura ya maoni kuhusu mpango wa kunusuru uchumi wa nchi hiyo …

Matokeo mechi za leo; Simba hoi, Ligi Kuu Zanzibar yasimamishwa

TIMU ya Simba ya Dar es Salaam imetoka droo na Moro Utd yaani (3-3), katika mchezo uliopigwa jijini Dar es Salaa. Yanga imefanikiwa kuifunga Polisi ya Dodoma (1-0), huku Azam FC ikitoshana nguvu na Toto Africa Mwanza kwa kutoka (1-1) mjini Mwanza. JKT Ruvu na Ruvu Shooting (1-1). Azam FC tayari imerejea jijini Dar es Salaam kwa mapunziko ya wachezaji …

Pinda ataka wakurugenzi 16 waadhibiwe

*Ni wa wilaya za Ludewa, Chamwino, Kondoa, Iringa na Shinyanga Na Mwandishi Maalumu WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Wakurugenzi wa Halmashauri 16 nchini ambao wamekiuka makubaliano na Mahakama ya kurejesha michango ya Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa watachukuliwa hatua za kinidhamu. Ametoa kauli hiyo leo Novemba 2, 2011 wakati akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri …