Watakiwa kulea watoto na si kutegemea ma-house girl

Na Anna Nkinda, Maelezo WAZIRI wametakiwa kutokufuata mambo ya utandawazi bali waweke mkazo katika jukumu la kuwalea watoto wao kwa misingi na maadili ya Kitanzania na siyo jukumu hilo kuwaachia mabinti wa kazi peke yao (ma-house girl). Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wazazi, walimu na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini …

Wizara ya Elimu kuwawajibisha wanaofaulisha kinyemela

Na Janeth Mushi, Arusha NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo amesema Serikali ipo katika mchakato wa kuandaa waraka utakaosambazwa kwa wakaguzi wa Kanda, Waratibu wa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Msingi nchini, ambapo wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza watatakiwa kuwa ni wale waliofaulu kwa haki. Naibu Waziri, Mulugo amesema hayo jana kwenye …

Ferguson asherekea miaka 25 akiwa Man U

MENEJA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anasherehekea miaka 25 na timu hiyo. Sir Alex Ferguson akisherehekea miaka hiyo 25 akiwa na Timu ya Man United amesema hatua hiyo ni kama hadithi nzuri. Katika miaka hiyo yote mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 70 ameisaidia Man kushinda Kombe la Premier mara 12, Kombe la FA mara tano na Ligi ya …

Nigeria yashambuliwa

WATU takriban 30 wamekufa katika shambulio kwenye mji mmoja Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Taarifa zinasema, Siasa Walioshuhudia tukio hilo Damaturu, Mji Mkuu wa Jimbo la Yobe, wanasema mabomu kadhaa yaliripuka jana usiku na magari kadha yaliteketea. Hapo jana pia mashambulio yalifanywa na watu waliojitolea mhanga katika Mji wa Maiduguri, shina la kikundi cha Waislamu wenye msimamo mkali la Boko Haram. …

Mama Kikwete achangisha zaidi ya mil 45.4 kuwasaidia wagonjwa watoto wa saratani

Na Joachim Mushi MKE wa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete leo jijini Dar es Salaam amechangisha sh. milioni 45.4 kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa chini ya miaka mitano na zaidi wanaoungua ugonjwa wa saratani nchini. Fedha hizo zilichangishwa baada ya Mama Salma kuongoza matembezi ya mshikamano yalioanzia Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia katika …