KOZI ya ukocha kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia kesho (Novemba 7 mwaka huu) hadi Novemba 20 mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TFF kupitia kwa Ofisa Habri wake, Boniface Wambura amesema makocha 30 ndiyo wanaoshiriki …
Nadir Haroub aenguliwa kikosi cha Stars
BEKI wa kati wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Nadir Haroub ameondolewa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena. Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Boniface Wambura aktika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo amesema; Haroub ameondolewa baada ya kuumia kifundo …
Kikwete ngoma nzito
Sitta, Nape wasubiri huruma yake BUNDI mharibifu anazidi kuinyemelea CCM hali inayotishia mgawanyiko mkubwa miongoni mwa makada na wanachama wa chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika.Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka jana, CCM imejikuta kwenye malumbano mazito miongoni mwa makada wake, yanayochangiwa kwa kiasi kikubwa na mitazamo tofauti katika uendeshaji wa chama na utekelezaji wa misimamo inayotolewa na chama …
Msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
MSIMAMO WA LIGI KUU 2011-2012
Serikali inakamilisha mpango wa vijana kujiunga na JKT- Rais Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali inakamilisha mipango ya kuanzisha upya utaratibu wa vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria kama ilivyokuwa zamani. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania iko tayari kutoa uzoefu wake wa jinsi ya kuendesha JKT kwa Zimbabwe ambayo nayo inaangalia jinsi ya kuanzisha …
Pinda awataka wazazi nchini waache uongo
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wazazi wenye uwezo wa kulipia watoto wao katika Vyuo Vikuu waache kusema uongo kwani kwa kufanya hivyo wanawakosesha watoto wa maskini kupata mikopo wanayostahili. Ametoa kauli hiyo leo Novemba 5, 2011) wakati akiwahutubia washiriki wa mahafali ya pili ya Chuo Kikuu cha St. John’s yaliyofanyika kwenye chuo hicho mjini Dodoma. Jumla ya wahitimu 1,002 walitunukiwa …