Ghasia zaendelea nchini Syria

WATU zaidi ya wanne wanahofiwa kuuwawa leo asubuhi nchini Syria, kwa mujibu wa wanaharakati wanaopinga serikali ya Rais Assad, na kwamba jana watu 27 waliuwawa. Taarifa kutoka Mashariki ya Kati, zinasema ghasia bado zinaendelea ikiwa ni siku nne baada ya Serikali ya Syria kutangaza kuwa imekubali mapendekezo ya amani ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kwamba itaondoa majeshi yake …

Kanisa lashambuliwa nchini Kenya

SHAMBULIO la guruneti kwenye kanisa moja mjini Garisa, Kaskazini Mashariki mwa Kenya, limewauwa watu wawili na wengine wawili kujeruhiwa. Mwandishi wa BBC mjini humo anasema, shambulio hilo lilitokea usiku, na hadi sasa haijulikani wahusika, wala lengo lao la kushambulia kanisa hilo. Vikosi vya usalama vimeanza uchunguzi, na mamia ya polisi wanaoenekana wakishika doria mjini humo. Kumefanywa mashambulio ya maguruneti ya …

Dk. Shein awataka watendaji kuwajibika kwa wananchi

Na Rajab Mkasaba, Ikulu-Pemba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa kila mwenye dhamana/utendaji kuheshimu dhamana yake kwa kuwajali walio chini pamoja na wale anaowahudumia. Alisema inasikitisha kusikia baadhi ya wafanyakazi huwatolea maneno yasioridhisha wanaowahudumia, hali ambayo huchangia wananchi kukata tamaa na kuanza kunungunika huku wakiilaumu Serikali yao. Alhaj Dk. …

Bingwa wa Vodacom Cycle Challenge 2011 Tanga apatikana

HASSAN Shariff amefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya mbio za baiskeli ya “Vodacom Tanga Cycle Challenge 2011” baada ya kumaliza mwendo wa umbali wa kilomita 140 akiwa mbele ya washiriki wengine. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Wakati Sports Promoter na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania yalishirikisha makundi matatu ambayo ni ya baiskeli zilizotengenezwa maalumu kwa michuano ambapo washiriki walipita Wilaya …