Serengeti Breweries yazindua tangazo la kampeni ya ‘pamoja tutashinda’

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imefanya hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila la kheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi yao na Chad. Sambamba na hafla hiyo, SBL imezindua rasmi tangazo la televisheni linalosema ‘TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA’. Akiwakaribisha wageni katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, …

Chuo Kikuu Norway kusaidia sekta ya afya Zanzibar

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar UONGOZI wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukland kiliopo Norway umeahidi kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kuiongezea misaada hospitali ya Mnazi Mmoja ili iendelee kutoa huduma zaidi kwa jamii. Hayo yalielezwa na Mkuu wa hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukland Profesa Steiner Kuinsland, akiuongoza ujumbe kutoka chuo hicho …

Sekondari ya Wama- Nakayama yasaidiwa vitabu 1,000

Na Anna Nkinda – Maelezo SHULE ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-NAKAYAMA iliyopo Rufiji mkoani Pwani imepokea msaada wa vitabu 1000 kutoka kwa Taasisi ya British Charity READ International ambayo inafanya kazi ya kukusanya vitabu nchini Uingereza na kuvigawa katika nchi za Afrika. Vitabu hivyo vimekabidiwa leo kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi …

Ikulu yawasaidia wasiojiweza kusherekea Idd el Hajj

Na Mwandishi Wetu VIKUNDI na vituo 14 vya watoto yatima na wenye ulemavu na wazee wasiojiweza vimenufaika na zawadi ya Sikukuu ya Idd El Hajj ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Watanzania jana, Jumapili, Novemba 6, 2011, waliungana na Waislam wengine duniani pote kusherehekea sikukuu hiyo. Vituo vilivyonufaika na zawadi hizo za Mheshimiwa Rais ambazo ni …

Rais Kikwete azungumza na mtoto wa Malkia

Na Mwandishi Maalumu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Novemba 7, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na Mtoto wa Malkia wa Uingereza, Prince Charles na Mkewe, Mama Camila, the Duchess of Cornwall. Prince Charles na ujumbe wake amewasili Ikulu, Dar es Salaam, kiasi cha saa 4:10 kwa ajili ya mkutano na mazungumzo na …

Mkutano wa mafunzo ya uongozi wafunguliwa Dar

PICHANI juu ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi (kulia) akiwa na Mchungaji, Dk. Bill Hybels (kushoto) wakimsikiliza Mratibu wa Mkutano wa Mafunzo ya Kuinua Uchumi, Ustawi wa Jamii na Uongozi Bora, Mchungaji, Peter Mitimingi uliofanyika leo kwenye hoteli ya Blue Pearl – Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri huyo amefungua …