Dk Slaa, Lissu mbaroni
WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KOSA LA KUFANYA MKUSANYIKA USIO HALALI, MBOWE ASAKWA Arusha KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu pamoja na wanachama wengine 25 wa chama hicho wamekamatwa na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali.Mbali na hao, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ametakiwa kujisalimisha …
Bingwa wa zamani wa ngumi uzito wa juu duniani afariki dunia
BINGWA wa zamani wa ngumi uzito wa juu duniani Joe Frazier amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi saratani ya ini, familia yake imesema. Taarifa zinazohusiana na masuala ya maswumbwi zinasema Frazier aliyejulikana kwa jina la Smokin’ Joe – alikuwa akitibiwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi mjini Philadelphia baada ya kugunduliwa anaugua saratani wiki kadha zilizopita. Bingwa huyo …
Rais Kikwete ataka ushirikiano na Uingereza kimaendeleo
Na Mwandishi Maalumu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameielezea Uingereza kama mshirika kakati (strategic partner) katika maendeleo ya Tanzania kutokana na miaka 50 ya ushirikiano na misaada ya maendeleo na ya kiufundi kutoka kwa nchi hiyo. Aidha, Rais Kikwete ametaka nchi zote mbili, Tanzania na Uingereza, kuongeza jitihada za kuvutia uwekezaji zaidi katika Tanzania kutoka Uingereza …
Stars kutua N’djamena leo kwa pambano
TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka Novemba 9 mwaka huu saa 9 alasiri kwa ndege ya Kenya Airways kwenda N’Djamena kwa ajili ya mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu. Msafara wa Stars wenye watu 40 ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella …
Rufani ya Michael Wambura yatupwa tena
KAMATI ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema haina mamlaka (jurisdiction) ya kusikiliza shauri lililowasilishwa mbele yake na aliyekuwa mgombea uenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Michael Richard Wambura. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kamishna Mstaafu wa Polisi Alfred Tibaigana, Wambura aliwasilisha rufani mbele yao akipinga uamuzi …