MAKAMU wa zamani wa Rais wa Benki ya Ulaya, Lucas Papademos ametangazwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Ugiriki, kufuatia siku kadhaa za majadiliano. Taarifa ya kuthibitishwa kwa nafasi ya Papademos imetoka katika Ofisi ya Rais wa Ugiriki. Taarifa zaidi zinasema kuwa viongozi wa vyama vikuu vitatu vinavyounda Serikali ya umoja wa kitaifa wamekuwa wakikutana na rais wa Ugiriki kujaribu kufikia …
Freeman Mbowe amburuzwa mahakamani Arusha
Na Mwandishi Wetu, Arusha MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe leo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha na kuunganishwa katika kesi inayomkabili Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. wilbroad Slaa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu na wenzao 25 ambapo anakabiliwa na mashitaka mawili. Mwendesha Mashitaka wa Serikali Haruna Matagane …
Stars yawasili Chad, Poulsen ataja kikosi cha kwanza
TIMU ya Taifa Stars ya Tanzania imewasili jana usiku mjini N’Djamena tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa kesho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya. Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura aliyoituma kwa vyombo vya habari leo, alisema timu hiyo imefikia hoteli …
Mbowe: Siwaogopi Polisi na Siwezi kuwakimbia
Na Mwandishi Wetu, Arusha MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo amezungumza na vyombo vya habari leo mjini Arusha na kudai hajawakimbia polisi na wala hawaogopi pale anapoungana na wanachama wake kudai haki zao. Mbowe ametoa kauli hiyo muda mfupi uliopita mjini Arusha na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi linawaongopea wananchi kwa muda mrefu dhidi ya viongozi wa CHADEMA. “Ndugu …
Tutahakikisha karafuu ya Zanzibar inaongezeka thamani- Dk. Shein
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufanya juhudi zote kuhakikisha zao la karafuu ya Zanzibar inaongezeka thamani na kuendelea kutambuliwa Kimataifa. Dk. Shein alieleza hayo leo huko Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa Wataalamu kutoka Shirika …