Dk. Shein azungumza na Saqr Al Qasimi

Na Rajab Mkasaba, Ras-Al-Khaimah RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na mwenyeji wake Kiongozi wa Ras-Al-Khaimah, Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi na kufanya mazungumzo yaliolenga kukuza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya pande hizo. Mazungumzo hayo yaliofanyika katika Kasri ya Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi lililopo mjini …

Pinda azindua ujenzi barabara ya Dodoma – Mayamaya

*Magufuli aahidi kulipa bil. 200 za wakandarasi wanaodai muda mrefu Na Martin Ntemo wa Wizara ya Ujenzi WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda leo Novemba 12 amezindua rasmi ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayoanzia Dodoma hadi Mayamaya yenye urefu wa kilometa 43.6. Kipande hicho cha barabara ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia mjini Dodoma kupita miji ya Kondoa, Babati, Arusha …

‘Magonjwa ya Polio, Surua kubaki historia Tanzania’

Na Magreth Kinabo- MAELEZO, Arusha SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema itahakikisha magonjwa ya polio na surua na mengineyo ambayo yanaweza kukingwa kwa chanjo yanatokomezwa ili yabaki kuwa historia. Kauli hiyo imetolewa leo mjini hapa na Makamu wa Rais DK. Gharib Bilal wakati akizindua Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua na utoaji wa matone ya Polio, Vitamin …

Clouds Media Group wachangia Damu Dar

Na Mwandishi Wetu WAFANYAKAZI kutoka Kituo cha Clouds FM na Televisheni ya Clouds leo wamejumuika na baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuchangia damu katika Benki ya Damu, Kituo Kidogo cha Damu Salama kilichopo Mnazi Mmoja. Zoezi hilo lililohamashishwa na Clouds Media Group limefanyika leo kuanzia mchana ambapo viongozi na wafanyakazi wamewaongoza baadhi ya wakazi wa jiji …