TFF yawataja waliochaguliwa kuongoza soka Mara
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limeweka wazi majina ya viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), baada ya uchaguzi ulifanyika Novemba 13 mwaka huu wilayani Rorya. Akitaja viongozi hao leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema katika uchaguzi huo uliendeshwa na …
Wachezaji 28 waitwa Kilimanjaro Stars
Na Mwandishi Wetu KOCHA Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ameteua wachezaji 28 kuunda kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji inatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 mwaka huu. Wachezaji walioteuliwa leo ni pamoja na Juma Kaseja (Simba), Deo Munishi (Mtibwa Sugar) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni Shomari …
Serengeti Breweries yawataja wanafunzi wanne bora iliyowadhamini Chuo Kikuu
Na Mwandishi Wetu BAADA ya kupokea maombi zaidi ya 250 ya wanafunzi wa kidato cha sita, kampuni ya bia ya Serengeti kupitia mpango wa ufadhili wa elimu ya juu unaoendeshwa na kampuni ya bia ya EABL imewachagua wanafunzi bora wanne ambao wamefanikiwa kupewa ufadhili wa elimu ya juu. Wanafunzi wote wanne walifanya vizuri sana kwenye mtihani wa kidato cha sita, …
Marais watatu wakutana kuijadili Somalia
MARAIS watatu wa Afrika Mashariki wamekutana katika Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi kuonesha umoja wao juu ya harakati za Kenya za kijeshi nchini Somalia. Mkutano huo kati ya rais wa Kenya, Mwai Kibaki, Yoweri Museveni wa Uganda na Sheikh Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia unafanyika ikiwa ni mwezi mmoja baada ya harakati hizo kuanza kuwasaka wanamgambo wa kundi la kiislamu …