JK awapa pole mapadre waliopoteza maisha kwa ajali
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Shirika la Makapuchini nchini Tanzania, Padre Wolfgan Peter, kuomboleza vifo vya mapadre wanne wa shirika hilo waliopoteza maisha yao katika ajali ya gari jana, Jumanne, Novemba 22, 2011 eneo la Ruvu kwa Zoka, Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Katika salamu hizo, Mheshimiwa Rais Kikwete …
Premium Serengeti Lager Has Won The Top Quality Award Across Africa
PREMIUM Serengeti Lager has won the top quality award among the Diageo products across Africa. According to Global Beer Technical Centre (GBTC) based in Dublin, Ireland, the brand won the accolades after a rigorous analysis. A statement issued in Dar es Salaam today by SBL which brews the beer brand said that the test is done after sending samples to …
Timu zilizowasili CECAFA Tusker Challenge Cup
TIMU zinazoshiriki CECAFA Tusker Challenge Cup zinaendelea kuwasili Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoanza Novemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo kwa vyombo vya habari ni kwamba; Somali na Djibouti tayari zimeshawasili. Ikifafanua zaidi taarifa hiyo iliyosainiwa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura inasema timu hizo zilitua …
Uchaguzi wa viongozi CECAFA Kesho
MKUTANO Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) utafanyika kesho (Novemba 24 mwaka huu) kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam. Moja ya ajenda katika mkutano huo utakaonza saa 4.00 asubuhi ni uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya CECAFA. Nafasi zinazogombewa ni tano; (Mwenyekiti na wajumbe wane wa Kamati ya …
Maonesho ya WEZA kufanyika Zanzibar Alhamisi
MRADI wa Kuwawezesha Wanawake Zanzibar (WEZA) kesho Alhamisi (tarehe 24/11, 2011) utafanya maonyesho ya kibiashara na utetezi katika hoteli ya Bwawani Zanzibar yatakayowashirikisha wadau 350 wakiwemo wajasiriamali walionufaika na mradi huo. Meneja wa Mradi wa WEZA, Rose Matovu amesema maonyesho hayo yatawapa fursa wanawake wa vijijini walionufaika na mradi wa WEZA zao kuonesha biashara zao na mbinu wanazotumia kufanya utetezi …