Tenga ashinda tena u-Wenyekiti CECAFA

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Tenga amechaguliwa leo (Novemba 24 mwaka huu) bila kupingwa baada ya mpinzani wake Fadoul Hussein wa Djibouti kutotokea kwenye uchaguzi. Kutokana na hali hiyo, mjumbe kutoka Uganda alitoa hoja …

Mkwasa ataja kikosi cha michuano ya Kombe la Tusker Chalenji

KOCHA Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 20 kwa ajili ya michuano ya Tusker Chalenji inayoanza kesho. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema wachezaji waliobaki na timu zao kwenye mabano kati ya 28 waliokuwa wameitwa awali ni pamoja …

Asante Kotoko ya Ghana kucheza na Yanga na Simba Desemba

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Soka ya Kumasi, Asante Kotoko ya Ghana inatarajiwa kuwasili nchini Desemba 9 tayari kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya kombaini ya Timu za Yanga na Simba siku ya Desemba 11 kwenye uwanja wa Taifa. Mchezo huo ni sehemu ya kukamilisha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na maandalizi yake yamekwisha …

Watanzania Ujerumani kushangweka na miaka 50 ya Uhuru!

Chereko chereko zitaanzia München hadi Berlin BENDI ya Ngoma Africa a.k.a FFU Desemba 10, 2011 inatarajia kutoa burudani ya kukata na soka kwa Watanzania wa Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) kuzinduliwa rasmi! Watanzania waishio Ujerumani wameanza shamra shamra za kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara, kwa kasi kubwa inayotingisha kila kona, sherehe hizo zinaanzia mjini München siku ya …

Maandamano yaendelea karibu na Tahrir

BADO kuna hali ya wasiwasi mjini Cairo huku waandamanaji wakiongeza kasi katika harakati zao za kutaka watawala wa kijeshi wajiuzulu. Kumekuwa na makabiliano katika barabara za mji huo huku idadi ya polisi wa kuzuia fujo ikiongezeka hasa katika jengo la wizara ya mambo ya ndani lililoko karibu na medani ya Tahrir. Waandamanaji wamekataa ahadi ya baraza la kijeshi linalotawala kuharakisha …