Na Joachim Mushi PROFESA wa Chuo Kikuu cha Elimu UDSM, Herme Mosha amesema Tanzania haiwezi kujivunia kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru ikiwa hadi leo asilimia 50 ya wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi wanafeli na huku asilimia 80 ya walimu wa shule za msingi ni waliopata daraja la tatu kushuka chini. Profesa huyo mkongwe kutoka tasnia ya elimu amesema hayo leo …
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuiwekea vikwazo Syria
JUMUIA ya Nchi za Kiarabu inajiandaa kuweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Syria, baada ya serikali ya nchi hiyo kushindwa kutekeleza sharti la kusaini makubaliano ya Jumuiya hiyo, ambayo yangeliruhusu waangalizi kuingia Syria. Tangazo hilo la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu limesababisha maandamano mapya nchini Syria. Waandamanaji wanaonesha uungaji mkono wao kwa wanajeshi walioasi, Free Syrian Army, ambao sasa wanadai …
Yahya Jammeh Rais mpya-Gambia
RAIS wa Gambia, Yahya Jammeh, ameshinda muhula mwengine wa miaka mitano, baada ya Tume ya Uchaguzi kumtanganza mshindi wa uchaguzi wa Alhamis iliyopita. Kiongozi huyo wa zamani wa mapinduzi ya kijeshi, amepata asilimia 72 ya kura, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Gambia. Mpinzani wake wa karibu, Ousainou Darboe, amepata asilimia 17, ambapo mgombea huru, …