Rais Kikwete awatunuku maofisa wa JWTZ
Na Mwandishi Maalumu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete, Novemba 26, 2011, ametunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Katika sherehe iliyofanyika kwenye Chuo cha Kijeshi Monduli, Arusha, Rais Kikwete ametoa kamisheni kwa maofisa wanafunzi 506 waliofanikiwa kumaliza mafunzo mafupi ya 27. Kati ya maofisa hao wanafunzi, 69 ni …
Dk. Bilal awataka Watanzania kuitumia vizuri elimu huria
Na Hilda Mhagama MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal amewataka Watanzania kuitumia fursa ya elimu huria inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kwani ni elimu bora ya juu inayotolewa kwa njia ya masafa. Dk. Bilal ametoa changamoto hiyo leo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mahafali ya 23 ya Chuo hicho yaliyofanyika …
Watanzania wasikate tamaa kupoteza mechi za mwazo-SBL
Na Mwandishi Wetu WADHAMINI wakuu wa Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) wamewataka Watanzania na wadau wa Soka nchini kutokata tamaa a timu za Tanzania kupoteza mechi zao za kwanza. Kauli hiyo imetolewa leo katika Uwanja wa Taifa na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Phraim Mafuru alipokuwa akizungumza na wana habari mara …
Tanzania yaanza vibaya Tusker Chalenji
Na Mwandishi Wetu MECHI ya Mashindano ya Tusker Chalenji kati ya Timu ya Tanzania, Kilimanjaro Stars na timu ya Rwanda imemalizika muda mfupi huku vijana wa Rwanda wakiibuka vinara wa mchezo huo. Rwanda imefanikiwa kushinda mchezo huo kwa kuilaza Kilimanjaro Stars 1-0, goli lililofungwa katika dakika 22 kipindi cha kwanza cha mchezo na nahodha wa Rwanda, Kalekezi Olivier. Kilimanjaro ambao …