Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeongeza idadi ya maprofesa, baada ya Baraza lake kuidhinisha kupandishwa vyeo kwa wahadhiri wake watano kuwa maprofesa kamili na maprofesa washiriki. Hatua hiyoilifikiwa katika kikao baraza hilo cha 204, kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Taaluma, Profesa Makenya Maboko, …
Arsenal presha juu kwa Fulham
Arsenal imeshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 1-1 na Fulham. Beki wa Arsenal Thomas Vermaelen alijifunga mwenyewe na kuipa Fulham bao la kuongoza katika dakika ya 65. Hata hivyo beki huyo alifuta makosa yake dakika nane baadaye kwa kusawazisha goli hilo kwa kupachika mpira wa kichwa kutokana na krosi iliyopigwa na Theo Walcott. Kipa wa …
Man U haina jipya kwa Newcastle
Manchester United imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Newcastle United. Sare hiyo imeifanya Newcastle iliyo katika nafasi ya tatu kuwa na pointi moja tu nyuma ya United iliyo nafasi ya pili nyuma ya United. Goli la Manchester United limefungwa na Javier Hernandez, huku goli ya Newcastle likifungwa na Demba Ba kwa mkwaju …
Takribani abiria mil. 6.5 hujisaidia hovyo kwa siku Tanzania
Na Joachim Mushi KILA ifikapo Novemba 19 mataifa mbalimbali ulimwenguni hufanya maadhimisho ya siku ya choo duniani. Kimsingi tunafanya maadhimisho ya siku hii ili kutambua umuhimu wa choo, kuwa na choo safi. Tanzania bado idadi kubwa ya familia hazina vyoo na hazitumii vyoo katika haja zake. Mfano kwa Jiji kama Dar es Salaam zaidi ya mabasi ya abiria 100 yenye …
Mihadhara ya kampeni yafutwa Congo
POLISI wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, wamepiga marufuku mikutano yote ya hadhara kwa sababu ya mvutano kuzuka baina ya pande zinazoshindana, siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo. Mkuu wa Polisi, Jean de Dieu Oleko, alisema mikutano yote imefutwa. Rais Joseph Kabila na wapinzani wake wawili wakuu, wakitarajiwa kufanya mikutano ya hadhara karibu-karibu. Mwandishi wa habari wa Reuters …
Chama Cha Mapinduzi njia panda
Chadaiwa kilikurupuka kujivua gamba, sasa kimekwama WAKATI CCM imemaliza vikao vyake vikuu vya maamuzi mjini Dodoma juzi bila kufikia kikomo cha dhana yake ya kujivua gamba, wasomi, wanaharakati nchini wamedai chama hicho tawala kilikurupuka ndiyo maana imeshindwa kutekelezeka. Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, wasomi, wanaharakati na wanasiasa hao walisema kuwa, chama hicho hakikufanya utafiti wa kina kujua …