Sarafu mpya ya Sudan Kusini yaibua utata kwa wafanyabiashara.

Ni zaidi ya miezi mitatu tangu Sudan Kusini ilipojitenga na Sudan na kupata uhuru wake mwezi Julai mwaka huu. Kama nchi mpya Sudan Kusini imekuwa ikianzisha taasisi mbali mbali za kitaifa kama vile benki kuu, mahakama, bunge na fedha zitakazo tumiwa katika nchi hii mpya. Lakini hata kwa kuzindua tasisi hizo, Sudan Kusini bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali, ikiwemo …

Sita wafariki katika ajali ya basi la wachezaji-Togo.

Watu sita walifariki baada ya basi lililokua likisafirisha wachezaji wa klabu ya mpira wa miguu Etoile Filante kudondoka katika korongo na kushika moto. Ajali hiyo ilitokea umbali wa maili 100 kaskazini mwa mji mkuu Lome wakati wachezaji hao wanakwenda kupambana na Timu nyingine katika michuano ya Ligi ya Togo. Pamoja na maofisa sita waliofariki, wengine 25 wamelazwa katika hospitali kwa …

Liverpool na Manchester City hakuna mbabe.

Bao la kujifunga la Joleon Lescott lilifuta jitihada za awali za Vincent Kompany kufunga bao wakati Manchester City walipoongeza wigo wa pointi hadi tano wakiendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Kandanda ya England. Liverpool yatoka sare na Manchester City bao 1-1 Mario Balotelli alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za manjano katika kipindi …

Cairo walazimisha Jeshi kukabidhi madaraka kwa Raia.

Maelfu ya watu wamekusanyika tena Medani Tahrir mjini Cairo, mkesha wa uchaguzi wa bunge uchaguzi wa kwanza tangu Rais Mubarak kuondolewa madarakani. Waandamanaji wanajaribu kuendelea na shime ya chagizo kutaka serikali ya kijeshi ikabidhi madaraka kwa raia. Mkuu wa serikali hiyo Field Marshall Hussein Tantawi, amesema uchaguzi wa bunge utafanywa kesho kama ulivopangwa, ingawa kuna ghasia za kisiasa. Alisema kuwa …

Chokochoko za Uchaguzi Mkuu Mashirika ya misaada yasikitishwa na ghasia za Congo

MASHIRIKA ya kimataifa, pamoja na Umoja wa Mataifa yamesema yanasikitishwa na ghasia zilizotokea jana katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ambapo watu wanne walikufa. Kiongozi mmoja wa upinzani anasema waliokufa ni zaidi na mpinzani mkuu, Bwana Etienne Tshisekedi, ametaka kukaidi amri ya kutofanya kampeni leo, mkesha wa uchaguzi kwa sababu alipanga kufanya mkutano huo wa …

JK akutana na CHADEMA, wawasilisha mapendekezo yao

*Wajumbe kukutana tena leo Na Mwandishi Maalum RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na ujumbe wa Serikali yake Novemba 27, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa CHADEMA umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa …