Rashid Matumla kuzichapa na Maneno Osward

Na Mwandishi Wetu MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni Desemba 25 mwaka huu, kuzichapa katika pambano lisilo la ubingwa. Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios ambaye ndiye muandaaji wa …

Hatma ya kesi ya Mbowe Desemba 20, 2011

Na Mwandishi Wetu, Arusha HATMA ya kesi inayowakabili viongozi wa juu wa CHADEMA, Katibu Mkuu, Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe itajulikana Desema 20, 2011- baada ya hakimu kumaliza usikilizaji wa pingamizi. Kesi hiyo pia inawajumuisha wabunge watatu pamoja na wafuasi wao 14, wa cha hicho. Jana mjini hapa wakili wa Serikali alikuwa akijibu hoja za pingamizi …

Dk. Shein amuapisha Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo mjini hapa amemuapisha Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar. Hafla ya kuapishwa kwa Katibu huyo, Mtoro Almas wa Zanzibar ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, …

Wahariri wawasili Moshi kushiriki uzinduzi wa kiwanda cha SBL

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limewasili mjini Moshi leo mchana kwa ajili ya kushiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Kiwanda kipya cha Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) kinachozinduliwa kesho mkoani Kilimanjaro. Akizungumza na dev.kisakuzi.com Katibu Mkuu wa TEF, Boniface Meena amesema jumla ya wahariri 36 kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini wamewasili tayari kwa …

Djibout mikono juu kwa Zimbabwe yalala 2-0

Michuano ya Mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP imendelea mjini Dar es Salaam nchini Tanzania ambapo timu mwalikwa wa mashindano hayo Zimbabwe imeifunga timu ya Djibout kwa magoli 2 -0 katika mchezo wa kundi A. Nazo Zanzibar na Burundi zimetoka sare bila kufungana katika mchezo wa pili wa kundi B. Ikiwa ni mechi yake …