RAIA wasiopungua 23 wameuwawa nchini Syria huku jumuiya ya nchi za kiarabu ikiiwekea vikwazo nchi hiyo. Uingereza imeipongeza hatua hiyo ikisema ni ishara kushindwa kwa utawala kutimiza ahadi zake hakutapuuzwa. Shirika la kutetea haki za binadamu la Syria, limesema raia saba waliuwawa na maafisa wa usalama katika mkoa wa kati wa Homs, akiwemo mmoja aliyepigwa risasi alipokuwa katika paa la …
Balozi wa Kenya afukuzwa Sudan
SERIKALI ya Sudan imemfukuza balozi wa Kenya nchini humo, kufuatia mahakama kuu ya Kenya kuamuru kukamatwa kwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir, anayetafutwa na mahakama ya kimataifa ya ICC. Balozi wa Kenya amepewa muda wa saa 72 awe ameondoka mjini Khartoum. Jaji wa mahakama kuu ya Kenya Nicholas Ombija alisema mwanasheria mkuu wa serikali na waziri wa usalama wa ndani …
Mataifa tajiri yawa kikwazo mkutano wa hali ya hewa-Durban.
WAKATI huu ambapo kikao cha viongozi kuhusu hali ya hewa kinaanza, baadhi ya nchi zinazostawi ulimwenguni ambazo zinahusika sana katika uchafuzi wa hewa zinajaribu kuchelewesha mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa hali ya hewa ulimwenguni. India na Brazil zimeungana na nchi tajiri katika kuitisha mazungumzo hayo yasifanyike kabla mwaka 2015, hili limeyaudhi sana mataifa madogo ya visiwani. Muungano wa Ulaya na …
Kenya yatoa hati ya kukamatwa kwa Bashir
Mahakama ya Kenya imetoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar al-Bashir juu ya madai ya uhalifu wa kivita mjini Darfur. Uamuzi huo umetolewa baada ya Kenya kumruhusu Bw Bashir kuzuru nchi hiyo mwezi Agosti ikipingana na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ya kutoa hati ya kukamatwa kwake. Jaji huyo alisema anatakiwa kukamtwa iwapo “atakanyaga Kenya” …
CHADEMA wakubaliana na Serikali, JK amaliza yaishe
Na Mwandishi Wetu CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hatimaye kimemaliza mvutano wake kati yake na Serikali ya CCM baada ya Rais Jakaya Kikwete kukubaliana na chama hicho katika vipengele kadhaa juu ya Sheria iliyopitishwa na Bunge kuandaa utaratibu wa kuelekea kuundwa kwa Katiba Mpya ya nchi. CHADEMA ambayo wajumbe wake kadhaa wamefanya mazungumzo na Rais Kikwete kwa siku mbili …