Magari ya Jeshi kutumika kubeba mahindi Tanzania

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali imefikia uamuzi wa kutumia majeshi yake ili kusomba mahindi yaliyolundikana katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na kuyapeleka katika mikoa yenye upungufu mkubwa wa chakula. Amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini kuwa kasi ya kusafirisha mahindi kwa njia ya reli peke yake ni ndogo na haikidhi mahitaji yaliyoko katika …

Mwekezaji si lazima atoke nje- Waziri Pinda

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema suala la uwekezaji hapa nchini haliwalengi watu wa nje tu bali hata wa ndani wanaweza kuwekeza hata kama ni kwa kiwango kidogo. Ametoa kauli hiyo jana usiku, wakati akizungumza na wakazi wa mikoa ya Rukwa, Ruvuma na mkoa tarajiwa wa Katavi katika chakula cha jioni ambacho aliwaandalia kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar …

Ngorongoro Heroes kwenda Botswana kesho

KIKOSI cha wachezaji 20 wa timu ya Taifa kwa vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na viongozi watano kinatarajia kuondoka Novemba 30 mwaka huu kwa ndege ya Precision Air kwenda Gaborone, Botswana. Ngorongoro Heroes itaondoka saa 20.20 usiku kupitia Johannesburg, Afrika Kusini kwenda huko kushiriki michuano ya umri huo ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa …

Waziri Pinda azindua kiwanda cha Bia ya Serengeti

Na Joachim Mushi, Kilimanjaro WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa huduma kwa jamii unaotolewa na kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL), kupitia kitengo chake maalumu cha kuwahudumia wananchi (CSR). Pinda alisema takwimu zinaonesha SBL kwa mwaka 2010, mbali na kulipa kodi ya bilioni 35.8, imetumia sh. milioni 350 kuwapatia maji safi na salama …

Zoezi la kuhesabu kura lagubikwa na mashambulio ya waasi- Congo

SHUGHULI za kuhesabu kura zinaendelea katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya uchaguzi mkuu hapo jana uliokumbwa na mashambulio ya waasi na machafuko katika baadhi ya vituo vya kupigia kura. Aidha watu waliokuwa wamejihami walishambulia kituo cha kupigia kura katika eneo la Lubumbashi na kuwauwa maafisa wawili wa Polisi na mwanamke mmoja. Pia walichoma magari manane yaliyokuwa yakisafirisha vifaa …