Toulambis – Primitive Tribe Meets White Man For The First Time (Video)

The Belgium anthropologist Jean Pierre Dutilleux discovered the unknown tribe called, The Toulambis, in Papua, New Guinea in 1993. The had never seen a white men before in their lives and according to them, the white men were “zombies”, living dead. You can clearly see their astonishment and fear when they are offered a helping hand by Jean Pierre.

Wanawake wabakaji Zimbabwe wafikishwa Mahakamani

Polisi wa Zimbabwe wanaamini kuna mtindo wa wanawake kuwabaka wanaume Zimbabwe , ili kutumia mbegu zao za kiume katika ushirikina kujitajirisha. Imechukuwa zaidi ya mwaka mmoja polisi kuwakamata wahusika na siku ya Jumatatu wanawake watatu walifikishwa mbele ya mahakama katika mji mkuu Harare kwa mashtaka ambayo yameishangaza nchi nzima. Mtu mmoja aliyepitia madhila hayo hakutaka jina lake kutajwa, alielezea yaliomkuta …

Upigaji kura waongezwa muda DRC

Muda wa upigaji kura umeongezwa na kuingia siku ya pili katika baadhi ya maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo sehemu ambazo upigaji huo haukufanyika siku ya Jumatatu. Maafisa wa uchaguzi walisema kuongeza muda huo kunaathiri takriban watu 400 katika nchi hiyo kubwa yenye vituo vya kupigia kura 63,000. Mbali na hatua hiyo kuchukua muda mrefu, upigaji kura huo uligubikwa …

Wahusika wa kashfa ya BAE TZ kushtakiwa

Kundi la wabunge kutoka vyama mbali mbali vya siasa nchini Uingereza limetoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi ya mtu yeyote aliyehusika katika kashfa ya ufisadi na rushwa kuhusiana na mauzo ya rada yaliyofanywa na kampuni ya vifaa vya ulinzi ya BAE Systems ya Uingereza. Kampuni ya BAE Systems tayari imekubali kulipa takriban dola millioni 46 kama fidia kwa Tanzania kwa …

Laurent Gbagbo apelekwa The Hague

Mwendesha mashtaka nchini Ivory Coast amesema kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Laurent Gbagbo, ameondoka kutoka mji wa Korhogo, kaskazini mwa nchi, na kwamba anasafirishwa hadi mahakama ya uhalifu wa kivita, mjini The Hague. Taarifa iliyosomwa kupitia televisheni ya kitaifa iliyotiwa saini na mwendesha mashtaka huyo, imesema kuwa mahakama ya ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa bwana Gbagbo wiki iliyopita, …

JK asaini muswada waliougomea CHADEMA

Na Mwandishi Maalumu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete hatimaye leo, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011, muswada ambao Chama cha Demokrasia na Maendeleo kiliugomea bungeni. Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema hatua hiyo ya kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya …