Mr Ebbo afariki dunia

MWIMBAJI nguli Tanzania aliyeibuka na staili ya bongofleva kwa ‘tune’ na staili ya Kimasai, Abel Rusheraa Motika, almaarufu – Mr Ebbo amefariki dunia. Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili alfajiri ya leo zinaeleza kwa Mr. Ebbo alifariki kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa kichomi kwa muda mrefu. Amefariki akiwa nyumbani kwa familia yake, maeneo ya Usa River, Arusha. Mwanamuziki huyo alifahamika …

Maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru

Rais Kikwete akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio hizo mwaka huu jijini Dar es Salaam jana. Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Walioketi toka kulia ni IGP Saidi Mwema, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange, Spika wa Bunge, Anne Makinda. Viongozi …

‘Watumishi umma wala rushwa ni watumwa’

WATUMISHU wa umma wanaokumbatia rushwa wamefananishwa na watumwa wanaoabudu wenye mali. “Mtumishi wa umma mla rushwa ni mtumwa anayeabudu wenye mali na kamwe hawezi kuwa na ufanisi kazini”, alisema Emmanuel Mlelwa, Kaimu Mkurungenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa. Mlelwa alizungumza hayo wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) kwa wakuu …

TBS yataja sababu za kuenea bidhaa bandia

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limesema kuenea kwa bidhaa duni na bandia nchini husababishwa na hali ya kupanda kwa bei za bidhaa halisi na zenye ubora unaotakiwa ikilinganishwa na bei za bidhaa duni na bandia. Taarifa hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo (TBS) , Charles Ekelege wakati akifungua semina kwa …

CHADEMA wamzuia JK kuunda ‘Tume ya Katiba’

*Wadai akiwapuuza atakiona cha moto Na Mwandishi Wetu CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete asiunde Tume ya kusimamia mchakato wa Katiba mpya hadi hapo marekebisho waliyokubaliana yatakapo ingizwa kama walivyokubaliana. CHADEMA kimesema kimeshangazwa na kusikitishwa kwa hatua ya Rais Kikwete kupuuza ushauri wao walioutoa hivi karibuni wakizungumza Ikulu wa kumtaka asitie saini Muswada wa Sheria ya …