Profesa Mwandosya atoboa siri ya afya yake

Na Magreth Kinabo, Maelezo na Bujo Ambosisye (MoW) WAZIRI wa Maji, Profesa Mark Mwandosya ambaye alikuwa amelazwa Hospitali ya Apollo, nchini India, amesema hajawahi kuugua na kulazwa hospitalini kwa miaka 34 akiwa mtumishi wa umma. Profesa Mwandosya, aliyasema hayo Desemba 03, 2011 akizungumza kwenye mkutano na watendaji wakuu, baadhi ya watumishi wa Wizara yake na waandishi wa habari kwa mara …

Mwanahabari Alfred Ngotezi afariki

TASNIA ya habari Tanzania imepata pigo kubwa baada ya jana kundokewa na mwandishi wa habari mkongwe, Alfred Ngotezi. Taarifa zilizopatikana jana usiku zinaeleza kuwa Ngotezi, alidondoka muda mfupi baada ya kutoka maliwato, akiwa katika moja ya hoteli za Mji wa Arusha na alifariki dunia muda mfupi baadaye. Inaelezwa kwamba alifariki saa 5:11 usiku “Ndugu yetu baada ya kurejea kutoka maliwatoni, …

Tanzania chup chup kutolewa Tusker Chalenji

Na Joachim Mushi TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) hatimaye imefanikiwa kuendelea ki-bahati nasibu na hatua ya pili katika Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji baada ya fufungwa mabao 2-1 na timu ya Taifa ya Zimbabwe jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kilimanjaro Stars imeponea chup chup baada ya kufanikiwa kufunga bao moja katika mchezo …

Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru

Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru; Sheria Kali zaidi yaja kuwakaba koo wafanyabiashara wanaotumia vipimo visivyo sahihi

Na Mwandishi Wetu Sabasaba WIZARA ya Viwanda na Biashara imesema mchakato wa marekebisho sheria ya vipimo unaendelea kwa lengo la kutoa adhabu kali kwa wafanyabiashara wanaotumia vipimo ambavyo sio sahihi. Hayo yamesemwa na Afisa Vipimo Mkuu daraja la pili, katika Wakala wa Vipimo Tanzania, Zainabu Kafungo katika maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Uwanja wa Mwalimu J …