Polisi wawili watiwa mbaroni kwa kumpa kichapo Diwani

Askari Polisi wawili wa kituo cha Mgeta wilayani Mvomero mkoani Morogoro, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumpiga Diwani wa Kata ya Kiteo, Exavery Msambara, kwa madai kwamba amekuwa akihoji utendaji wa kazi za polisi. Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Josephat Rugila, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Desemba Mosi, mwaka huu saa 4:00 asubuhi katika kituo cha Polisi Mgeta, …

Maambukizi ya VVU Jiji la Tanga yanatisha

Kiwango cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) katika Halmashauri ya Jiji la Tanga kimeongezeka kwa asilimia 8.7 zaidi ya kile cha kitaifa cha asilimia 5.7. Kiwango hicho ambacho kimeelezwa kuwa kimekuwa kikipungua kwa kasi ndogo sana, kimezidi hata kile cha mkoa ambacho ni asilimia 4.8. Akihutubia katika kilele cha Siku ya Ukimwi Duniani na ufunguzi wa maadhimisho ya miaka …

Zanzibar, Burundi wafungasha virago Tusker Chalenji

*Sudan, Rwanda wakata tiketi Nusu Fainali Na Mwandishi Wetu WAKATI timu za taifa za Sudan na Rwanda zikikata tiketi za kuingia Nusu Fainali ya Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji jana Timu ya taifa ya Zanzibar imeungana na Burundi na kuyaanga mashindano hayo baada ya kukubali kichapo katika michezo miwili ya jana. Mchezo wa kwanza timu ya Sudan ilifanikiwa kuingia …

Dk. Shein akabidhiwa ripoti ya uchunguzi Mv. Spice Islander

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, jana amekabidhiwa ripoti ya kuzama kwa Meli ya MV. Spice Islander na Tume ya Uchunguzi wa ajali hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Abdulhakim Ameir Issa. Mara baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais Dk. Shein alitoa pongezi kwa Tume hiyo kwa kazi …

Mr Ebbo azikwa na maelfu ya waombolezaji

Na Janeth Mushi, Arusha NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi, Goodluck Ole Medeye, jana ameongoza maelfu ya waombolezaji toka maeneo anuai nchini katika mazishi ya aliyekuwa mwanamuziki maarufu nchini Abel Loshilaa Motika “Mr Ebbo” (37) aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki. Mr Ebbo aliyefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu kwa muda wa miezi tisa …

JK atuma salamu za rambirambi NSSF

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau kutokana na kifo cha Mwandishi wa Habari Mkongwe, Alfred Ngotezi aliyekuwa akifanya kazi katika mfuko huo kama Ofisa Uhusiano Mwandamizi. Ngotezi aliyewahi kufanya kazi katika gazeti la Serikali la Daily News …