Na Mwandishi Wetu, Arusha JESHI la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Julius Masheri pamoja na Mkuu wa Usafirishaji (TO), Bakari Jabu kwa tuhuma za kughushi matumizi hewa ya mafuta. Kwa mujibu wa chazo chetu cha habari kinaeleza kuwa wanaohojiwa katika tuhuma hizo ni pamoja na wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Monduli …
Kimiti awataka Watanzania kutembelea Maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru
Na Tiganya Vincent, MAELEZO-Dar es Salaam MWANASIASA nguli na Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Paul Kimiti amewataka Watanzania kutembelea Maonyesho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ili kushuhudia viongozi anuai wazalendo walivyoleta mabadiliko ya kimaendeleo baada ya taifa kujitawala. Kimiti ambaye pia amewahi kuwa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za …
Makocha 40 kuwania leseni daraja ‘B’ CAF
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha majina ya makocha 40 wa Tanzania kushiriki katika kozi ya ukocha ya leseni B ya shirikisho hilo. Makocha wote waliopitishwa wana cheti cha ukocha cha ngazi pevu (advance). Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ni miongoni mwa makocha hao watakaoshiriki kozi hiyo itakayofanyika jijini …
Dk. Shein kufunga Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji
Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kufunga michuano ya 35 ya CECAFA Tusker Challenge Cup inayoendelea jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo Dar es Salaam, sherehe za ufungaji wa mashindano hayo yaliyoshirikisha mataifa 10 wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika …
Kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Brig. Gen Moses Nnauye
Brig. Gen M. Nnauye
Laurent Gbagbo afikishwa mahakamani
RAIS aliyeondolewa madarakani nchini Ivory Coast, Laurent Gbagbo amefikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Laurent Gbagbo anakuwa ni rais wa kwanza kukabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo, huku akiwa ameshtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu kwa kuhusishwa na umwagikaji damu uliotokea baada ya uchaguzi wenye utata mwaka jana. Gbagbo alipelekewa nchini Uholanzi wiki iliyopita. Kiongozi huyo …