Na Joachim Mushi TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars imetinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Malawi bao 1-0, katika mchezo mkali na wa kuvutia uliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Kilimanjaro Stars ambayo ilicheza kwa kujihami mchezo huo, mpaka inakwenda mapumziko, ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na mchezaji …
Spika Makinda azindua ripoti ya UN kuhusu haki za watoto
Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akitoa ujumbe wa umoja wa mataifa kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ongezeko la idadi ya watu, masual ya wanawake na watoto jana wakati wa uzinduzi wa ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki, idadi ya watu na masuala ya vijana leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Aron …
Dk. Shein ataka SUZA ibadilike kimaendeleo
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mazungumzo na Wajumbe wa Baraza na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), na kueleza kuna haja ya chombo hicho kubadilika kiutendaji kwa lengo la kukiendeleza na kukiimarisha chuo. Dk. Shein aliyasema hayo jana alipofanya mazungumzo na viongozi hao …
TAFFA kuondoa urasimu bandarini
Na Mwandishi Wetu CHAMA cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) kinacho shughulikia shehena zote zinazo ingia na kutoka nchini kwa njia ya bandari, anga na mipakani kimesema kimepanga kujenga ushirikiano na taasisi anuai inazofanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha inaongeza na kuinua pato la Serikali kupitia shughuli zao. Kauli hiyo imetolewa jana na rais wa chama hicho, Stephen Ngatunga alipokuwa …
Asilimia 44 ya wanawake hunyanyaswa kijinsia- Waziri
Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Sheria na Katiba Tanzania, Celina Kombani amesema kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizoendeshwa zimebaini kuwa asilimia 44 ya wanawake nchini wamekutana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa waume zao. Kombani ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua kampeni ya kupinga Unyanyasaji wa Kijinsia. Pamoja na hayo Kombani amesema vitendo vya …