Maadhimisho Miaka 50 ya Uhuru Tanzania Bara yafana

*Maonesho ya shughuli za JWTZ yavutia wananchi Na Joachim Mushi SHEREHE za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru zimefana kwa kiasi kikubwa baada ya kupambwa na maonesho ya Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi. Sherehe hizo zilizoongozwa na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete zimeambatana na maonesho …

FFU wa Ngoma Afrika wawasili Berlin!

*Ni kwa kufanya onesho la Sherehe za miaka 50 ya Uhuru UMOJA wa Watanzania nchini Ujerumani (UTU) unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Desemba 10, 2011 Berlin! Kikosi Kazi cha Ngoma Africa band a.k.a FFU, kimeshatua mjini Berlin kwa kazi ya kutumbuiza katika hafla ya uzinduzi huo. Kikundi hicho cha wasanii kinatarajiwa kushambulia jukwaa kwa burudani murua katika kusherekea miaka 50 ya uhuru …

Wateja wa M-PESA kupokea fedha kutoka nje ya nchi kupitia Western Union

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Western Union na Vodacom Tanzania zimezindua huduma mpya ambapo itawafanya wateja wao kupokea fedha zao kupitia huduma ya M-PESA. Kwa mara ya kwanza wateja wa simu za mkononi wa Vodacom nchini watakuwa na uwezo wa kupokea fedha kutoka nje ya nchi moja kwa moja kupitia huduma ya Vodacom M-PESA. Huduma ya Mobile Wallet ambayo ndio …

SMZ kudhibiti ufujaji Airport Zanzibar

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali imeamua kujenga Uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa lengo la kukuza uchumi, huku akiweka bayana taratibu zinazochukuliwa kudhibiti ufujaji mapato kiwanjani hapo. Dk. Shein aliyasema hayo leo mara baada ya ziara yake ya kutembelea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa …