Waziri Mkuu Pinda kufunga Maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru Dar

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda Desemba 12, 2011 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shughuli maalum ya kufunga Wiki ya Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru itakayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari Dar es Salaa na …

Rais Kikwete: Umoja Daima

ASAMEHE WAFUNGWA 3000, WABAKAJI WAENDELEA KUSOTA VIONGOZI mbalimbali wa ndani na nje ya nchi jana, waliungana na Watanzania kusherehekea kumbukumbu ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara kwenye tukio la kihistoria lililofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Sherehe hizo zilihudhuriwa na marais kutoka nchi mbalimbali, mawaziri wakuu, mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na viongozi mbalimbali wa …

Kabila atangazwa tena mshindi wa urais DRC

ALIYEKUWA Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila ametangazwa tena kuwa ni mshindi wa urais wa taifa katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa za Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo, Kabila ameshinda kwa asilimia 48, huku mpinzani wake mkuu, Etienee Thisekedi akiwa na asilimia 32.33 na Vital Khemere akiambulia asilimia 7.74. Awali ilitangazwa matokeo hayo yangelichelewa …

Wabunge wawachapa 5-1 Wawakilishi Zanzibar

*Wabunge wanawake nao wawachakaza Wawakilishi netibali Na Joachim Mushi TIMU ya mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania leo imeiadhibu bila huruma Timu ya mpira wa miguu ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar (BLW) baada ya kuichapa mabao 4 kwa 1. Timu ya Bunge ambayo iliongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (Mb) akicheza …

Waziri Pinda azindua mradi wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika

Na Mwandishi Maalum MRADI wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika wenye kuenzi mchango wa Tanzania na nchi nyingine za Afrika katika harakati za ukombozi wa Bara hilo, umezinduliwa jijini Dar es Salaam Alhamisi Des. 8, 2011 na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Chini ya mradi huo, kumbukumbu, alama, nyaraka , maarifa na taarifa mbalimbali kuhusu harakati za ukombozi zitakusanywa …