UJUMBE wa Kimataifa wa wasimamizi wa uchaguzi umetamka kuwa ni kweli uchaguzi uliofanywa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ulikuwa na dosari kadhaa hivyo si wa kutegemewa. Hata hivyo, tayari Rais Kabila alishinda katika uchaguzi huo. Kituo cha Carter kimesema kuwa uchaguzi huo umetiwa dosari, kwa kutotayarishwa sawasawa, na pengine ulikuwa na udanganyifu. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa matokeo ya vituo …
Urusi kwachafuka, maelfu waandamana
MAELFU ya wananchi nchini Urusi wameandamana katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo wakishinikiza kurudiwa kwa Uchaguzi wa Bunge uliofanywa Jumapili iliyopita nchini humo. Taarifa kutoka ndani ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Moscow, zinasema maandamano makubwa yamefanywa katika Mji huo, ambako mwandishi wa BBC, anasema maelfu ya watu wako katika medani, ng’ambo ya pili ya mto, mkabala na Ofisi za …