TFDA wazindua maabara ya kimtandao ya ubora wa bidhaa

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imezindua mradi wa kimtandao utakaofanya kazi ya kudhibiti na kulinda ubora wa vifaa anuai kwenye maabara yake ambayo hutumika kuchunguza na kubaini maradhi ya binadamu. Akizindua mradi huo jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya alisema mradi huo utasaidia kugundua kwa …

Miaka 50 ya Uhuru, Ubalozi wa Tanzania wafanya kweli Ujerumani

*Ngoma Africa Band wawakivutio kwa waheshimiwa DESEMBA 9 na 10, 2011 Watanzania waishio Ujerumani na nchi jirani wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani, walijikuta wakilitingisha Jiji la Berlin katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Taarifa zinasema sherehe hizo zilizoongozwa na Balozi, Ngemela na maofisa wengine wa ubalozi akiwemo, Ali Siwa zilianzia katika Ukumbi …

Kilimanjaro watakiwa kutumia fursa kujiletea maendeleo

Na Aron Msigwa – MAELEZO WANANCHI wa Mkoa Kilimanjaro wametakiwa kutumia fursa zilizopo katika mkoa huo ukiwemo Mlima Kilimanjaro, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kujiletea maendeleo. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia alikuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Cleopa …

JK katika mazungumzo na Balozi wa Uturuki

Rais Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Uturuki aliyemaliza kufanya kazi nchini Dk. Sander Gurbuz aliyekwenda kumuaga leo Jumanne Desemba 13, 2011 Ikulu jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)

Rais Kikwete afanya mazungumzo na Benki ya AfDB

Na Mwandishi Maalumu RAIS Jakaya Kikwete leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi kazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dk. Tonia Kandiero. Dk. Kandiero amefika Ikulu kujitambulisha baada ya kuanza kazi hapa nchini mwezi Mei, mwaka huu kuchukua nafasi ya Dk. Sipho Moyo ambaye alimaliza muda wake hapa Tanzania. ADB ni moja …