Waziri Mkuu Tanzania ahimiza uwekezaji kikanda Kilimanjaro

Na Mwandishi Maalumu, Kilimanjaro WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amesema Mkoa wa Kilimanjaro unaweza kuwa kitovu cha maendeleo katika kanda ya Kaskazini kama ukijipanga vizuri na kutumia fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa huo. Ametoa kauli hiyo leo mchana Desemba 15, 2011 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Maendeleo Mkoa wa Kilimanjaro (Kilimanjaro Development Forum – KDF) unaofanyika …

Rais Kikwete aenda Uganda kuhudhuria mkutano wa ICGLR

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameondoka nchini leo, Desemba 15, 2011, kwenda Kampala, Uganda ambako ataungana na viongozi wenzake wa nchi za Maziwa Makuu kuhudhuria Mkutano wa Mwaka wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Nchi za Maziwa Makuu wa International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR). Kwa mujibu wa taarifa …

Kambi ya Ngumi Ilala kumuandaa bondia Ubwa Salum

KAMBI ya Mchezo wa Ngumi ya Mkoa wa Kimichezo wa Ilala, Dar es Salaam, inamuandaa bondia Ubwa Salum kwa ajili ya pambano lake dhidi ya bondia Mustafa Dotto, litakalofanyika Desemba 25 mwaka huu. Akizungumza jana Dar es Salaam Kocha Msaidizi wa Kambi Ilala, Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema pambano hilo litakuwa kati ya mapambano yatakayotangulia katika pambano kali linalowakutanisha mabondia …

Wanajeshi wa Marekani waondoka Iraq

RAIS wa Marekani Barack Obama maeadhimisha kumalizika kwa vita vya Iraq kwa kupongeza “mafanikio yasiyo ya kawaida” kwa vikosi vya Marekani katika mapigano ambayo yalipingwa na wengi. Katika hotuba yake kwenye eneo la Fort Bragg mjini Carolina Kaskazini, aliwapongeza wanajeshi wale waliohudumu na hata kufariki dunia wakiwa vitani, pamoja na jamii zao. Wanajeshi wa Marekani wa mwisho kutoka nchini Iraq …

Marekani yasema uchaguzi DRC ulikuwa na dosari

MAREKANI imesema uchaguzi uliofanyika hivi karibuni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ulikuwa na dosari nyingi, hivyo kutaka mchakato wa tathmini urejewe upya. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yamempa, Rais Joseph Kabila ushindi wa asilimia 49 dhidi ya asilimia 32 alizojipatia kiongozi wa upinzani na mpinzani mkuu wa Kabila, Etienne Tshisekedi. Taarifa kutoka Marekani zinasema, hata hivyo matokeo hayo yamekosolewa …