JK asema suala la ukosefu wa ajira Afrika linahitaji majibu

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana wa Afrika ni jambo kubwa, linalohitaji majawabu makini na ya haraka na hatua kubwa zisizohitaji kucheleweshwa tena kutoka kwa viongozi wa Bara hilo. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa uharaka wa kupata majawabu ya tatizo hilo yanatokana na ukweli kuwa kila nchi …

Mahakama Kuu Tanzania yasajili mawakili 315 wapya

Na Mwandishi wetu MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imewasajili na kuwatambua mawakili wapya 315. Zoezi hilo la usajili limefanyika jana jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande. Akizungumza katika hafla hiyo, Jaji Mkuu Chande amesema bado sekta ya Mahakama inakabiliwa na changamoto ya ucheleweshaji wa mashauri mbalimbali yanayowasilishwa pamoja na ukosefu wa uelewa wa sheria …

Dk. Shein awataka ZAWA kutoa elimu kwa wananchi

Na Rajab Mkasaba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kutoa elimu kwa wananchi juu ya tatizo la upungufu wa maji katika vianzio vyake pamoja na kueleza athari zinazosababishwa na hali hiyo na kupelekea baadhi ya maeneo kukosa huduma ya maji. Dk. Shein aliyasema hayo leo …

SBL wamleta bingwa wa ‘cocktail’ Tanzania

Na Japhet ole Lengine YULE bingwa wa kuchanganya vinywaji vikali duniani maarufu kama (cocktail) kutoka London Uingereza, Kenji Jesse, sasa ametua hapa nchini kwa udhamini ya Kampuni nya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji cha Smirnoff kinachosambazwa na kampuni hiyo. Mtaalam huyo wa kuchanganya vinywaji vikali vya aina mbalimbali na kutengeneza kinywaji chenye ladha ya kipekee, ameendesha semina maalum kwa watoa …